Meneja
Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande (mwenye suti ya
damu ya mzee) akinyoosha kidole kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadick (wa pili kulia) sehemu korofi za kutiririsha
maji machafu barabara ya Morogoro kati kati ya jiji.
Na Damas Makangale
WATENDAJI
wa Mamlaka za Maji Safi na Taka, Manispaa, Halmashauri, Wakala wa
Barabara na Mabasi yaendayo kasi wameshauri kuwa na utaratibu wa
kuwasiliana na kushirikiana kwa pamoja ili kuleta tija katika usombaji
taka katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza
na mwandishi wetu, kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh
Said Meck Sadick, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw.
Anthony Mark Shayo amesema kuwa tatizo la jiji la Dar es Salaam ni
watendaji wa mkoa hawana mawasiliano ya kutosha katika utendaji kazi wa
kila siku.
Shayo
alizungumza hayo kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya
kugagua hali ya usafi katika maeneo kadhaa pamoja na kuangalia maeneo
korofi katika kutitirisha maji machafu kwenye mitaro kadhaa kati kati ya
jiji.
“tatizo
kubwa katika jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa jiji, manispaa,
wakala wa barabara, Tanesco na mamlaka za maji safi na taka kutokuwa na
utaratibu wa kuwasiliana katika utendaji kazi wa kila siku katika
kuboresha usombaji wa taka kwenye jiji la Dar,” amesema Shayo
Meneja
Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande akiwaonyesha baadhi
ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said
Meck Sadick na Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu baadhi ya mashimo
(Potholes) ambayo ni hatari kwa wananchi watembea kwa miguu baada ya
ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.
Shayo
alilisisitiza kwamba katika utendaji kazi wa jiji kama la Dar
inahitajika ushirikiano wa dhati kati ya wadau wa kusomba taka na
watendaji wa manispaa pamoja na jiji ili kuweka mkoa wa Dar es Salaam
katika hali safi wakati wote.
Amesema
kuwa ingawaje tatizo kubwa la uchafu linasababishwa na miundombinu
mibovu ya barabara na maji hasa kuelekea katika dampo kuu la mkoa
sehemu ya Pugu Kinyamwezi, Gongo la Mboto.
Shayo
ambaye kampuni yake inajishughulisha na usombaji wa taka ngumu na
nyepesi katika mkoa wa Dar es Salaam amesema kwamba mamlaka zinazohusika
kwa kushirikiana na wadau lazima watoe elimu ya kutosha kwa wananchi
kuhusu umuhimu wa kuhifadhi taka.
“sehemu
ya dampo la Pugu Kinyamwezi. inahitajika kampuni ya ujenzi yenye uwezo
wa kuboresha miundombinu ya barabara kuelekea kwenye dampo ili kupunguza
foleni ya magari ya taka na kuongeza tija ya kazi katika eneo husika,”
aliongeza
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick akiongoza msafara wa
baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika kuangalia hali ya
usafi na miundombinu ya maji na barabara jijini Dar.
Kwa
upande wake, Minael Mshanga Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, amesema jiji
limejipanga kufanya ukarabati wa miundombinu ya barabara kuelekea dampo
ili kuongeza kasi ya magari yanayokwenda kumwaga taka katika dampo hilo.
“hivi
tupo katika hatua za mwisho na tumempata mkandarasi wa kuja kujenga na
kutengeneza miundombinu ya barabara kuelekea katika dampo pamoja na
kutengeneza mataa katika eneo husika ili kazi ya kutupa taka ifanyike
usiku na mchana,” amesema Mshanga.
Aliongeza
kwamba jiji lina mpango wa kuanza kushirikiana kwa karibu na
wakandarasi wazalendo katika kuleta ufanisi wa usombaji taka ili kuzuia
magonjwa ya mlipuko katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mbunge
wa Ilala, Hassan Zungu akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said
Meck Sadick wakati wa ziara ya ghafla ya kugagua hali ya miundombinu ya
maji na barabara kati kati ya jiji la Dar.
Baadhi
ya magari ya wakazi wa jiji yakipita kwa taabu katika madimbwi na
mashimo ya maji machafu kati kati ya jiji la Dar es Salaam.
Viongozi
wa mkoa wa Dar es Salaam wakijadili moja ya sehemu korofi kati kati ya
jiji karibu na Haidery Plaza ambapo kipindi cha mvua maji taka
yaliyochanganyikana na kinyesi yanatuama kwa kipindi kirefu ambapo
hakuna mfereji wala mtaro wa maji machafu.
Mashimo ya miaka nenda rudi yasiyopatiwa ufumbuzi lakini baada ya ziara yatarekebishwa.
Mkuu wa mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akitoa ushauri kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midala (mwenye tai nyeusi).
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Udhibiti taka kutoka jiji, Enezael Ayo (kushoto)
akifafanua jinsi magari ya taka yanavyomwaga taka katika dampo kuu la
Pugu Kinyamwezi jijini Dar wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tirima Enterprises, Robert Ngeleshi akizungumza changamoto
na matatizo ya mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar ambao
waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo
akielezea jambo kwa mkuu wa mkoa wakati wa kuhitimisha ziara hiyo katika
maeneo ya dampo Pugu Kinyamwezi.
Moja ya Bull dozer linalorekebisha barabara likiwa limeharibika kutokana na miundombinu mibovu katika dampo la Pugu Kinyamwezi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji, Minael Mshanga (kulia kwa Mkuu wa Mkoa) akitoa
ufafanuzi wa matatizo na changamoto za usombaji na utupaji taka katika
dampo la Pugu Kinyamwezi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick akiagana na wakandarasi wa usombaji
taka na watendaji wa jiji. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Raymond Mushi.
wako waume wababa kwa vijana ambao hawana kazi wangepewa kila mtaa atleast 2 people kusimamia usafi...Wawajibishe wale wanaotupa taka ovyo na kuwatoza fine...Nahakika vijana wangepewa kazi hiyo jiji lingekuwa safi...Iwe kama Moshi kuchungana na Fine kwa kwenda mbele uchafu kwishney
ReplyDelete