Wednesday, March 26, 2014

KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII YA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE YAPITISHA MPANGO WA TIBA KWA KADI


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (Kulia) akichangia mada wakati wa wa kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kuendesha kikao hicho, Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi (katikati) na Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).

Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi akiendesha kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Meneja wa Bima ya Afya – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto) akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) wakati wa kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni mgeni rasmi aliyekaribishwa kuendesha kikao hicho, Diwani wa Kata ya Ngombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi (katikati) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
 Mwenyekiti wa Vibindo, Gaston Kikuwi akiongoza ni Wajumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) kutoa pongezi wa waheshimiwa madiwani kuweza kupokea kwa mikono miwili mpango wa Tiba Kwa Kadi (TIKA).
Wajumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Wajumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT) wakifuatilia kwa makini.
Waheshimwa Madiwani wakifuatilia kwa makini kikao hicho, toka kulia ni Diwani wa Kata ya Kwamsisi, Mheshimiwa Nassoro Hassan, Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Mji Korogwe, Mheshimiwa Neema Isack pamoja na Diwani wa Kata ya Magunga, Mheshimiwa Mariam Ngonyani (Mama Maji Marefu).
Mratibu wa Ukimwi (CHAC) wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya afya ya halmashauri ya mji wa Korogwe, Tanga (CHMT), akichangia mada. 
Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Mji Korogwe, Mheshimiwa Neema Isack akitoa msimamo wake katika mada iliyokuwa ikijadiliwa.
Diwani wa Kata ya Kwamsisi, Mheshimiwa Nassoro Hassan akiongea machache wakati akichangia mada. Pembeni ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale.
Diwani wa Kata ya Kwamsisi, Mheshimiwa Nassoro Hassan akiongea machache wakati kikao cha Kamati ya Afya ya halmashauri ya mji huo (CHMT) pamoja na Madiwani wa Kata mbali mbali za Korogwe, Tanga kujadili mchakato wa kubadirisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha pili kimefanyika leo Machi 26, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Tanga. Pembeni ni Afisa Matekelezo na Uratibu wa Bima ya Afya, Singida Bw. Issaya Shekifu (kushoto) na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Korogwe, Jerry Mwakanyamale (kulia).
Mwenyekiti wa Vibindo, Gaston Kikuwi akijadili jambo na Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Mji Korogwe, Mheshimiwa Neema Isack.

No comments:

Post a Comment