Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.
Eneo hilo la Tengeru ambalo zamani lilikuwa likimilikiwa na
Hortculture Tanzania Ltd linatazamiwa kujengwa mji wa kisasa
utakaojulikana kama Satelite City.
Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa NHC Nehemea Mchechu
aliwaambia wajumbe wa kamati ya ardhi ,amaliasili na mazingira kuwa
tayari NHC imenunua ekari 600 ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi za
kitanzania bilioni 5.
Nyumba 300 zinatarajiwa kujengwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo
kadharika kutajengwa maduka makubwa ,shule pamoja na vituo kwa ajili
ya huduma kwa jamii na kwamba ujenzi wa nyumba nyingine 300 utafuati.
Mchechu alisema ujenzi huo hauta athili kwa namna yoyete ile uoto wa
asili ikiwemo miti katika eneo hilo na kwamba wanataegemea kuacha
sehemu ya Mikahawa iliyopo hapo kama kumbukumbu.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu
akisalimiana na mbunge wa jimbo la Arumeru Joshua Nassar wakati kamati
ya bunge ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea eneo ambalo
linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu
akiteta jambo na mkurugenzi wa shirika la hifadhi la
taifa(TANAPA)Allan Kijazi alipotembelea eneo ambalo linatazamiwa
kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City eneo la Tengeru
Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu
akitoa burudani ya nyimbo kwa wajumbe wa kamati ya Ardhi,maliasili na
mazingira ilipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa
kisasa ujulikanao kama Satelite City eneo la Tengeru Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu
akitunzwa na Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya wakati mkurugenzoi
huyo alipokuwa akitoa burudani ya Nyimbo ya Bob Marley.
Wajumbe wengine walishindwa kujizuia wakaamua na wao kuonesha vipaji vyao.
Kazi nzuri Bwana Mchechu, ila Angalia waist line!
ReplyDelete