Sunday, February 9, 2014

LIGI DARAJA LA KWANZA : POLISI MORO WAICHAPA BUKINAFASO 3-1

Kikosi cha Timu ya Bukina Faso ya Morogoro Kilichoanza
Waamuzi wa Mchezo huo Pamoja na Manahodha wa Timu zote..
Kikosi cha Timu ya Polisi Morogoro Kilichoanza,
Moja ya Hekaheka katika Lango la Timu ya Polisi Morogoro baada ya Kupigwa Shti Kali Langoni kwao.
Mshambuliaji wa Bukina Faso Saidi Manga ambaye aliifungia timu yake  bao dakika 51 akishangilia Mbele ya mashabiki wa timu hiyo ..

Mashabiki wa Timu ya Bukina Faso wakishangila Kwa Nguvu Mara baada ya Kupata Goli la Kuongoza Katika Mchezo wa Ligi daraja la Kwanza.
Mashabiki wa Timu ya Polisi Morogoro wakiwa hawaaamini Kinachotokea uwanjani.

Mchezaji wa Polisi Moro Fanuel Simon Akifunga Goli la Kusawazisha Kwa njia ya Mkwaju wa Penati Dakika ya 81 ya Mchezo mara baada ya Mabeki wa Bukina Faso walipomchezea Rafu Mshambuliaji wa Polisi Morogoro na Ndipo Mwamuzi alipoamuru Mkwaju wa Penati.
Beki wa Polisi Morogoro Akiangalia Mbinu za Kuondosha hatari zilizokuwa zinaelekezwa langoni kwao.
Polisi Morogoro katika dakika ya 87 baada ya Beki wa Bukina Faso Kujifunga Mpira wa Kona Uliopigwa Vizuri na  Nahoda wa Polisi Moro.
Wachezaji wa Polisi Morogoro wakishangilia Ushindi wao.
 Mshambuliaji wa Bukina Faso Ally Mayuki[kulia] akitafuta mbuni za kumtoka beki wa Polisi Morogoro Teru Ally
 Mayuki akifumua shuti baada ya kutoka beki Teru Ally  Hata hivyo shuti hilo lilidakwa na kupi wa Polisi Bakari Abdul

Ligi Daraja la Kwanza ilianza Kutimua Vumbi jana Ambapo Katika  dimba la uwanja wa Jamhuri Ulipigwa Mchezo wa Kati ya Polisi Morogoro na Bukina Faso  ya Morogoro.

Katika Mchezo Huo Uliokuwa na Upinzani Mkalia Ulimalizika  Polisi Moro walishinda bao 3-1.
Burkina faso walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupa bao dakika 51 kupitia kwa Said Manga , Dakika 10 za mwisho polisi waliliandama lango la Burkina faso na kufanikiwa kupata pelnati dakika 81 ambapo Fanuel Simon alipiga Pelnati hiyo kuifundi na kuisawazishia timu yake. 
Hadi 90 za kawaida  zilikuwa sare ya bao 1-1 ambapo dakika za nyongeze Polisi Moro Walifanikiwa Kupata Magoli 2

No comments:

Post a Comment