Monday, February 10, 2014

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah akiwasili kwa boti katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Kigoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe Bibi. Noelia Myonga, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmoud Mgimwa,Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Abdulkarim Shah na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bibi. Hadija Nyembo.
 Katikati ya Msitu wa Gombe Wajumbe wa Kamati wakipumzika kwa muda wakiwa njiani kuelekea katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe huku wakimsikiliza Mkuu wa Hifadhi Bibi Noelia Myonga (kushoto).
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Abdulkarim Shah akiwaongoza wenzake kuelekea katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe katika Hifadhi ya Gombe.
 Wajumbe wa Kamati wakiwa katika picha na baadhi ya watumishi katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe.
 Baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati wakati wa kuagana mara baada ya kumaliza ziara yao hifadhini.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kagongo wilayani Kigoma madarasa manne yaliyojengwa na Hifadhi za Taifa kupitia Hifadhi ya Gombe.
 Madarasa manne katika Shule ya Sekondari ya Kagongo wilayani Kigoma yaliyojengwa na Hifadhi ya Taifa ya Gombe.

No comments:

Post a Comment