Askari polisi wakikusanya nguo za ndani katika soko la Meiomoria
wakati wa operesheni ya kukamata wauzaji wa nduo hizo zilizopigwa
marufuku.
Askari polisi akimsindikiza mwanamke mmoja ambaye jina lake
halikufahamika mara moja baada ya kukutwa akiuza nguo za ndani
zilizopigwa marufuku katika soko la Meimoria mjini Moshi.
Mmoja wa wauzaji wa nguo za mitumba katika soko la Meimoria akiwa
amejificha chini ya meza ya kuuzia nguo kukwepa askari polisi pamoja
na maofisa wa shirika la viwango Tanzania (TBS) wakati wakifanya
operesheni ya kukamata wauzaji wa nguo za ndani.Mwananmke huyo alitoka
chini ya meza baada ya kubembelezwa na wenzake hata hivyo wakati
askari polisi akimtaka kwenda kupanda gari la polisi mwanamke huyo
alikimbilia tena chini ya meza hiyo,askari polisi wakalazimika
kumucha.
Mmoja wa wauzaji wa nguo za ndani akiingia kwenye gari la polisi baada
ya kukutwa akiuza nguo za ndani.
Askari polisi akimuhoji mmoja wa wauzaji wa nguo za ndani,juu ya uwepo
wa nguo hizo katika stoo yake ya kuhifadhia Marobota ya nguo za
mitumba.
Operesheni ikiendelea Stoo moja baada ya nyingine ambapo jumla ya
Marobota matano yalikamatwa na kisha kuteketezwa katika dampo la
Kaloloeni.
Mmoja wa wauaji wa nguo za ndani,akiwa mikonoi mwa polisi muda mfupi
baada ya jaribio la kuwakimbia askari kushindikana.
Marobota yaliyokamatwa katika soko la Meimoria yakipakiwa katika gari
tayari kwenda kuchomwa katika dampo la Kaloleni.
Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jami,Moshi.
Jamani sasa wanakataza watu wasifanye biashara ya kuuza mitumba nguo za ndani .Je kuna mtu anayelazimishwa kununua?Kwa nini inapigwa marufuku?Ninavyojua mimi kwenye hiyo mitumba kunapatikana vitu vingine vipya kabisa.sasa hawa watu wakale wapi? Je walala hoi ambao hujipatia chupi au sidiria kwa sh 1000 wataweza za 10000 sh ?Kuna vingi vya kukataza hamjaona wahusika ila mnafuata wafanya biashara wadogo wadogo_?jela mnazijaza kwa bila kuangalia nani anapasae huko.Mnatuogopesha kurudi kwetu maana ni mauza mauza.
ReplyDelete