Sunday, December 1, 2013

Sheikh Kilemile: Tukilea Watoto Vizuri, Tutapata Taifa la Waadilifu

   Ustaadh Ally Abrahaman Muki, ambaye ni Mwl Katika Kituo Cha Madrassa Mukkarramah & Nursery School akitunukiwa cheti pamoja na vifaa vya Kufundishia na Mgeni Rasmi Sheikh Suleiman Amran Kilemile vilivyotolewa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kituo hicho Jana.
   Kiongozi wa Kikundi cha Kinamama cha Ahbaabur Rasuul, Ukhty Samia akipokea zawadi ya Jola ya Kitambaa kama sehemu ya Uwezeshwaji kiuchumi kwa akina Mama uliotolewa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation kwa ajiri ya unifomu za Wanafunzi wa Kituo Hicho.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation walipokuwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa Kituo cha Madrassa Mukarramah & Nursery School kilichopo Kipala Mpakani – Mkuranga, Pwani.
  Sehemu ya Nyumba ya Mwalimu wa Kituo Cha Madrassa Mukarramah & Nursery School kabla ya Kupata Ufadhili wa Kuiboresha kama inavyonekana hapa chini kwa kuwa ya Kisasa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation.
  Sehemu ya Nyumba ya Mwalimu wa Kituo Cha Madrassa Mukarramah & Nursery School baada ya Kupata Ufadhili wa Kuiboresha kama inavyonekana hapa chini kwa kuwa ya Kisasa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation.
 Ustaadh Ally Abrahaman Muki akiwa katika sehemu ya Mapumziko na wageni ya Nyumba mpya  iliyofadhiliwa na taasisi ya Kalamu Education Foundation ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji maadili mema kwa watoto na Vijana.
  Sheikh Suleimani Amran Kilemile Akifanya Uzinduzi wa Kituo cha kisasa cha Madrassa Mukarramah & Nursery School Kilichopo Kipala Mpakani-Mkuranga Pwani.
 Madrasa
  Kutoka Kulia, Sheikh Suleiman A. Kilemile Mwenyekiti wa Umoja wa wanazuoni wa Kiislam Tanzania, Ustaadh  Ally Abrahaman Muki wa Madrassa Mukarramah & Nursery School na Sheikh Ally Mbwela wakiwa pamoja na Akina mama wa kikundi cha Ahbaabur Rasuul cha Madrassa Mukarramah & Nursery School wakati wa Uzinduzi wa Kituo hicho.
  Sheikh Suleiman Amran Kilemile wakifurahia jambo na Ustaadh Ally Abrahaman Muki na Mwl Ally Mbwela muda mfupi baada ya uzinduzi wa Madrassa Mukarramah & Nursery School Mkuranga Pwani kilichojengwa na Kalamu Education Foundation. Sheikh Kilemile alikuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo.
   Baadhi ya wanafunzi wa Madrassa Mukarramah & Nursery School ya Mkuranga, Pwani wakiwa wenye matumaini makubwa baada ya Kupata Kituoa cha Kisasa cha Elimu ya Dini na Shule ya Awali.
1.       Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania Sheikh Suleiman Amran Kilemile akisisitiza Umuhimu wa Kuwapa Malezi bora watoto ili kujenga Taifa la watu waadilifu  na wenye utu wakati wa uzinduzi wa Kituo Cha  Madrassa Mukarramah & Nursery School  Kipala-Mpakani, Mkuranga Pwani Kilichojengwa na Kalamu Education Foundation.

2 comments:

  1. Masha Allah, Madrassa inapopewa kipaumbele , Jazakallah kheir

    ReplyDelete
  2. nawapongeza sana kwa maendeleo haya wengine waige

    ReplyDelete