Thursday, December 12, 2013

NSSF YANOGESHA SIKU YA FAMILIA BULYANHULU

KAHAMA, Shinyanga

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa kiasi cha shilingi milioni 2, fulana 450 na kalenda 180 kwa uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko Kakola, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kufanikisha sherehe za Siku ya Familia ya Wafanyakazi wa mgodi huo.

Siku ya Familia 'Bulyanhulu Family Day 2013' ya Bulyanhulu Gold Mine ilifanyika mgodini hapo Desemba 8 mwaka huu, ambako pamoja na mambo mengine, NSSF ilitoa elimu ya kina kwa wachimbaji, maofisa na wafanyakazi wengine mgodini, kuhusiana na mafao na huduma zingine za shirika.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga, shirika hilo lina wanachama zaidi ya 3000 katika mgodi wa Bulyanhulu, ambao kupitia siku hiyo walijumuika pamoja, ikiwamo kufurahi na kutanua uelewa wao juu ya huduma zinazotolewa na NSSF.

Katika sherehe hizo, licha ya wafanyakazi na viongozi kutambuana na kubadilishana mawazo, NSSF pia ilitoa elimu ya kutosha kuhusu huduma zake, ikiwamo ya mafao mbalimbali yatolewayo na shirika hilo kwa wanachama wake wakati wakiwa kazini na baada ya kustaafu.

Mafao yanayotolewa na NSSF ni Fao la Matibabu, Kuumia Kazini,Uzazi, Mazishi, Urithi, Ulemavu, Uzee pamoja na Mikopo kwa Wanachama kupitia Saccos.
 Meneja Mkuu wa Bulyanhulu Gold Mine, Peter Buger (kushoto)  akimshukuru, Kaimu Meneja wa NSSF Kanda ya Kahama, Lusato Ernest baada ya kupokea msaada wa sh. milioni 2 kwa ajili ya kufanikisha ya sherehe za siku ya familia iliyofanyika Kakola wilayani  Kahama mkoani Shinyinga. 

 Mwakilishi wa NSSF Kakola, Barry Mwaga akitoa maelezo kuhusu athari za kujitoa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Umuhimu wa Fao la kuumia Kazini kwa wafanyakazi wa migodini.  
Kaimu Meneja wa Kanda ya Kahama wa NSSF, Lusato Ernest akifafanua jambo kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NSSF na mafao yake saba ambayo ni Fao la Matibabu, Kuumia Kazini,Uzazi, Mazishi, Urithi, Ulemavu, Uzee pamoja na Mikopo kwa Wanachama kupitia Saccos.
Mfanyakazi wa mgodini akifurahia kalenda ya NSSF ya mwaka 2014 waliyopatiwa wakati wa sherehe ya Siku ya Familia.
Ofisa Matekelezo wa NSSF, Said Mkwizu akielezea kuhusu mafao ya uzazi. 
 Kaimu Meneja wa Kanda ya Kahama wa NSSF, Lusato Ernest akifafanua jambo kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NSSF na mafao yake saba.
Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment