Monday, December 30, 2013

MTEMVU AIPIGA JEKI TIMU YA NETIBOLI YA TEMEKE QUEENS MASHINDANO YA KOMBE LA TAIFA 2013

 Mbunge wa Temeke, ambaye pia ni Mlezi wa timu ya netiboli ya Temeke Queens, Abbas Mtemvu, akimrejeshea Kombo la ubingwa Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Kibira lililokuwa linashikiliwa na mabingwa watetezi wa michuano ya Taifa Cup, Temeke Queens. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo kwenye Uwanjawa Taifa Dar es Salaam.
 Mtemvu akimkabidhi kocha wa Temeke Queens, Amina Mussa fedha kwa ajili ya posho za wachezaji na viongozi wa timu hiyo inayoshiriki michuano hiyo.

 Mtemvu akiwa na wachezaji wa timu ya Temeke Queens mabingwa watetezi wa mashindano hayo.
 Mwanaidi Ngubege wa Temeke Queens (kushoto) akijiandaa kufunga goli dhidi ya timu ya Mkoa wa Katavi.
 Lillian Sylidion wa Temeke akidaka mpira

  Mchezaji Sekela Dominick (kushoto) wa timu ya Temeke Queens akigombea mpira wa juu ya Rose Israel wa timu ya Mkoa wa Katavi katika mashindano ya kuwania Kombe la Taifa (Taifa Cup) siku ya ufunguzi wa michuano ya mchezo wa netiboli, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Temeke Queens ilishinda 58-27. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Benchi la wachezaji wa timu ya Mkoa wa Katavi
Kocha Amina Mussa wa Temeke akitoa mawaidha kwa wachezaji wakati wa mapumziko

No comments:

Post a Comment