Wednesday, December 11, 2013

Mkwere wa Mizengwe aula ubalozi wa kampuni ya simu bila jina

Muigizaji wa vichekesho  kwenye kundi la Mizengwe Hemedi Khalida maarufu kama Mkwere ameangukiwa na neema ya ubalozi wa kuhamasisha upatikanaji wa jina la  kampuni ya simu iliyoziduliwa bila jina. Kampeni hiyo itafanyika kupitia simu na mitandao mbalimbali ambapo wananchi wanatakiwa kuipatia jina kampuni hiyo. Mbali na hayo Mkwere atapata nafasi ya kupita mitaa mbalimbali akiwahimiza wananchi kupiga kura.

Sekta ya mawasiliano ya simu Tanzania na Afrika Mashariki imepata matumaini mapya kufuatia kuingia kwa kampuni mpya ya simu ya kipekee, ya ubunifu, yenye kuamini jamii, na yenye ushindani kuliko zote, kuzinduliwa bila jina.  

Pamoja na ahadi yake ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mawasiliano ya mtandao wa simu, kampuni hiyo mpya kwa wakati mmoja imezindua pia kampeni ya kiubunifu inayotambulika kwa jina la “Tupe Jina” itakayofanyika kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi katika simu kwa lengo la kuipa fursa Afrika Mashariki kuichagulia jina bora kampuni hii kwa kupiga kura.  


Hii ni kampuni ya kwanza ya simu Afrika Mashariki ambayo kweli inajali na haigopi kuamini watu, na hakuna kampuni nyingine inaweza kuthubutu kufanya hivyo. Hakuna kampuni yoyote duniani iliyoweza kuzinduliwa bila jina na kutoa jukwaa kwa kampeni ya kusisimua kabla ya jina kuwekwa hadharani.


“Tupe Jina” ni kampeni itafanyika  kwa awamu mbili katika mtandao, ujumbe wa simu na mtandao wa kijamii wa facebook. Katika awamu ya kwanza, Afrika Mashariki inapaswa kuteua majina ambayo wanapenda hii kampuni mpya iitwe.

Mshirki anaweza kuchagua jina kwa kuingia katika mtandao wa Unaweza kuteua jina  kwa njia ya magogo kwenye mtandao wa www.giveusaname.net au kutuma ujumbe wa simu ukiambatanishwa na jina analopendekeza kwenda namba  15678 au aingie katika mtandao wa www.facebook.com/giveusaname. Katika awamu ya pili ya kampeni, jopo litatathmini majina yote na itatoa majina matano ambayo yamependekezwa mara nyingi zaidi, ya kipekee na yenye ubunifu.

 Baada ya hapo Afrika Mashariki watapiga kura kwa ajili ya kupata jina bora moja ambalo hatimaye litakuwa jina la kwanza la kampuni hii ya mawasiliano ya simu ambayo daima itakuwa ya kwanza ya Kiafrika Mashariki. Mshindi katika kampeni hii, mtu ambaye atakuwa amechagua jina ambalo hatimaye litakuwa la kampuni atajishindia muda wa bure wa kupiga simu za ndani na SMS bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Zawadi zingine zitakuwa simu za kisasa za ‘smartphone’ na kompyuta za kiganjani (tablets) kwa washiriki wa kampeni hii ya “Tupe Jina”.

Kutokana na wataalam kutabiri kuongezeka kwa pato la taifa la Tanzania kutoka asilimia 4 hivi sasa hadi asilimia 7 mwaka 2015, sekta ya mawasiliano ina nafasi kubwa ya katika ukuaji wa uchumi katika miaka ijayo na kampuni hii mpya ya mawasiliano ya inawakilisha sura ya kasi hii kubwa ya ukuaji.

Tanzania inabaki kuwa ni moja ya nchi zenye kiwango cha kuingiza simu chini ya asilimia 50 kufikia Juni 2013, jumla ya matumizi ya mawasiliano ya simu nchini humo ni chini ya wastani kwa nchi za Afrika.

Hii kampuni mpya ya simu kwa umuhimu mkubwa itawekeza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wateja wake kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu kwa watu wa Tanzania katika sekta ya afya na hasa katika tiba za kimtandao na vituo vya elimu ya masafa.

Hii tafsiri yake ni kwamba kuwekeza idadi kubwa ya faida katika kuwezesha Afrika Mpya kuzingatia ongezeko la watumiaji wa mawasiliano ya simu, na zawadi bora ambayo kampuni hii inatarajia katika miaka ijayo ni kukuza sekta ya afya.

Baada ya kampeni ya “Tupe Jina” wananchi wa Tanzania watapata nafasi ya kupeleka namba zao wanazopendekeza kabla ya kutangazwa na kuwekwa hadharani kwa jina la kampuni.

No comments:

Post a Comment