Thursday, December 19, 2013

MAMA SALMA APOKEWA KWA SHANGWE BAADA YA KURUDI NA TUZO YA UONGOZI KUTOKA DUBAI

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja kumpoke
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CEL
 Hongera sana mama....
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ofisi za WAMA, ambako mamia ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya kumpongeza baada ya kurudi na Tuzo ya uongozi aliyopokea huko Dubai
 Baadhi ya wananchi walioshiriki mapokezi ya Mama Salma wanaonekana wakimsikiliza wakati alipokuwa akiwahutubia katika viwanja vya WAMA
 Ngoma ikirundika
 Sehemu ya waliojitokeza kumpokea na kumpongeza Mama Kikwete
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi waliofika kumpokea aliporejea kutoka Dubai tarehe 19.12.2013.  Mama Salma alienda huko kupokea Tuzo ya uongozi ulitukuka kutokana na kazi anazofanya kupitia Taasisi yake kwa ajili ya elimu kwa wanaotoka katika mazingira magumu, afya ya mama na mtoto pamoja na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wananchi waliofika kumpokea aliporejea kutoka Dubai tarehe 19.12.2013.  Mama Salma alienda huko kupokea Tuzo ya uongozi ulitukuka kutokana na kazi anazofanya kupitia Taasisi yake kwa ajili ya elimu kwa wanaotoka katika mazingira magumu, afya ya mama na mtoto pamoja na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha TUZO wananchi waliokusanyika katika viwanja vya WAMA kwa ajili ya kumpongeza baada ya kuwasili nchini
 Viongozi wa Girl Guides nao walishiriki katika kumpongeza Mama Salma baada ya kurejea nchini akitokea Dubai alikoenda kupokea Tuzo ya Uongozi itolewayo kwa wanawake kutoka nchi za Afrika, Mashariki ya Kati na Asia waliofanya kazi kubwa za kushughulikia masuala muhimu kwa maendeleo ya watu hasa katika elimu, afya na uwezeshaji.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza na wananchi waliofika kumpokea kwenye ofisi za WAM
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiongea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Raymond Mushi wakati wa shamrashamra za kumpokea Mama Salma baada bya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kupokea TUZO ya uongozi uliotukuka. Tuzo hiyo hutolewa na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi, (CELD). PICHA NA JOHN  LUKUWI

No comments:

Post a Comment