Sunday, December 1, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHEREHESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM, LEO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.
 Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya  Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye  maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
 Maandamano ya Siku ya Ukimwi duniani
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja kati ya Vitabu vya Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Mussa, baada ya ya kuzindua mpango mkakati huo wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi, Mashine za CD4 kwa ajili ya Kanda za Juu Kusini, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment