Monday, December 23, 2013

KITUO CHA POLISI OYSTERBAY KUBOMOLEWA NA KUJENGWA MADUKA YA KISASA

Na Sufiani Mafoto
 Kituo cha Polisi cha Oysterbay, pamoja na nyumba za Polisi wanaoishi katika Kambi hiyo, vitabomolewa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa maduka ya kisasa mfano wa Mlimani City ujenzi unaotarajia kuanza mwakani. Tayari baadhi ya askari waliokuwa wakiishi katika Kambi hiyo wameshapewa 'Notisi' ili kuhama katika nyumba zao na wengine kubomoa wenyewe majengo waliyokuwa wamejengwa kwa mabati katikati ya kambi hiyo ambayo walikuwa wakiishi, ambapo wengi wao waliokuwa wakiisha katika nyumba za mabati wamekwishabomoa nyumba zao na kuhama, huku baadhi wakiwa wamesalia wakisubiri awamu ya pili. Askari hao wameelekezwa kuhamia katika nyumba mpya zinazojengwa eneo la Kunduchi. 

Baadhi ya askari wamelalamikia utaratibu huo wa kuhamishwa katika eneo hilo, hali ya kuwa pamoja na kubomolewa nyumba zao na Kituo cha Polisi, lakini imeelezwa kuwa kitajengwa Kituo kipya kikubwa katika eneo hilo ambacho kitajengea upande wa pili barabara ya Ubalozi wa Marekani.

Kinachowafanya baadhi ya askari kulalamikia utaratibu huo ni kutokana na kujengwa tena kituo kikubwa katika eneo hilo, lakini nyumba za askari zikiondolewa na kutotakiwa kuwepo tena, ambapo askari wote watapewa nyumba Kunduchi na kila atakayekuwa zamu atalazimika kusafiri ili kufika kazini, jambo ambalo limeonekana ni usumbufu na hasa pale itakapotokea dharula za kikazi.

Kamera ya Sufianimafoto, ilibahatika kukatiza katikati ya kambi hiyo na kushuhudia nyumba nyingi zikiwa tayari askari wameshahama huku zile za mabati zikiwa zimebolewa na askari wakiwa tayari wamehama huku wengine wakiendelea na zoezi la ubomoaji na kuhamisha mizigo yao kwa awamu.
 Hili ni jengo maarufu kwa jina la 'BANGALOO' ambalo mara nyingi hufikia wale askari wanaotoka Depo yaani askari wapya wanaoanza maisha, ambao wengine hunogewa nalo na kubakia humu kwa maisha yao yote ya kiaskari, hili likiwa bado kubomolewa na baadhi ya askari wakiwa bado wanaendelea kuishi.

Mbele ya jengo hili kulikuwa na nyumba za mabati za askari ambazo tayari zimekwishabomolewa kama inavyoonekana pichani.
 Baadhi ya nyumba za askari waliokwisha hama askari na kuachwa wazi.
 Mmoja wa wanafamilia za Polisi akiwa nje na mizigo wakati wakipakia baadhi kuhamishia katika makazi mapya huko walikoelekezwa.
 Tafakuri...........
 Eneo hili kimebaki kibanda hiki tu ambacho mwenyeji wake bado anaendelea kuhamisha vitu taratibu kutokana na wingi wake.
 Eneo hili linalopakana na ukuta wa Tanesco, ndilo limeelezwa kuwa ndipo litakapokuwepo Geti kubwa la kuingilia katika Maduka hayo.
 Utafikiri ni 'Bushi' flani hivi kubwe ni Oysterbay Polisi Kambini hapa tayari vibanda vimeshabomolewa.
 Hii ndiyo hali halisi ya mazingira ya ndani ya Kambi ya Oysterbay Polisi kwa sasa wakati nyumba kibao zikiendelea kubomolewa.
 Hata hii njia inayotoka Morocco kukatiza katikati ya kambi hii na kutokea upande wa pili wa Mafret hadi Msasani haitakuwepo tena.
 Ubomoaji ukiendelea...
 Upande huu ndiyo pekee ambao bado hawajaanza kubomoa....
 Zitabomolewa zote hizi...
 Eneo la Kituo upande wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

No comments:

Post a Comment