Sunday, December 1, 2013

ASAS NA MSOWOYA WAKEMEA SIASA ZA MAKUNDI NDANI YA UVCCM MKOA WA IRINGA





 makada wa CCM wakiwa  wamembeba  juu mwenyekiti mpya wa chipukizi  mkoa wa Iringa 

 kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa  Salim Asas kushoto akimkaribisha mwenyekiti wa  chipukizi mkoa Enock Luhala mara  baada ya kutangazwa mshindi  katika uchaguzi mkuu wa Chipukizi mkoa
 Kamanda  wa UV CCM ambae  alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi  wa Chipukizi mkoa wa Iringa  Salim Asas akiwa na viongozi  wa UVCCM mkoa Tumain Msowoya  mwenyekiti wa umoja  huo kushoto na mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoa Enock Luhala kulia
 Kamanda  wa   UVCCM mkoa  wa  Iringa  Salim Asas kushoto na mwenyekiti  wa  UVCCM mkoa wa Iringa  Tumain Msowoya wakiwa wamewapakata  wajumbe  wa mkutano mkuu wa Chipukizi mkoa  wa Iringa mara baada ya uchaguzi 

NA  FRANCIS GODWIN BLOG

KAMANDA  wa  umoja wa  vijana  wa  chama  cha mapinduzi (UVCCM)  mkoa  wa  Iringa Salim Asas  amewataka   UVCCM mkoa  wa Iringa  kujipanga  vema  kujenga  chama katika  jimbo la Iringa mjini  na kuepuka  siasa  za makundi .

Asas alisema  kuwa ili  kuwa na chama imara  ni vema jumuiya  hiyo ya vijana na jumuiya  nyingine ndani ya CCM mkoa wa Iringa kufanya kazi kama  timu moja  ya ushindi  na kuepuka  kuendesha  siasa  za makundi ambazo hazina faida  ndani ya CCM.

Asas ambae  alikuwa mgeni rasmi katika  uchaguzi  wa chipukizi mkoa  wa Iringa alitoa kauli hiyo  juzi wakati wa mkutano  uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Iringa mjini 

Alisema  kuwa  kila jumuiya ndani ya CCM kuna  makundi isipo kuwa   Chipukizi ambao  wao  wameendelea  kuungana kwa  kuwa  kundi  mmoja  bila ya  kujigawa kama  zilizo jumuiya  nyingine.

Katika  hatua  nyingine Asas  alitaka kuanzia  sasa  UVCCM mkoa  wa Iringa  kuhakikisha  inafanya kazi kwa  kushirikiana na Chipukizi badala ya kuendelea  kuwabagua .

Alisema mara  baada ya  uchaguzi huo sasa mkoa kuandaa mpango  wa  kuwatembeza  Chipukizi bungeni , katika  hifadhi  mbali mbali za Taifa na maeneo mengine kwa ajili ya kujifunza kwa gharama  za  UVCCM mkoa .

"Hivi   jumuiya  ya wazazi  tuna makundi , vijana tuna makundi , UWT  tuna makundi ila chipukizi  wao  hawana makundi...sasa ombi langu vijana  tuige mfano  wa chipukizi kwa  kuepuka makundi na badala  yake  tuungane pamoja  kuwa kundi moja  la CCM kwa ajili ya kuimarisha  chama"

Alisema  hivi  sasa   chama  hasa  vijana wanapaswa kuungana pamoja  ili  kukijenga  zaidi  chama katika  jimbo la Iringa mjini   na kuwa  iwapo  chama kitakuwa imara  zaidi muda  ukifika  wa  kumtafuta mgombea  hata  kama atawekwa nani atashinda  kwa  kishindo badala ya  kuendesha  siasa  za makundi ambazo  zinakigawa chama.

Awali  mwenyekiti wa UVCCM mkoa  wa Iringa Tumain Msowoya  akimkaribisha kamanda huyo  wa UVCCM kuzungumza  katika mkutano  huo alisema  kuwa  mwaka  kuna  uchaguzi  wa serikali za mitaa  hivyo anachoomba vijana kujiepusha na makundi ya kisiasa .

Kwani  alisema kuwa  vijana kama kisima  cha  kutoa  viongozi  baadhi ya  wagombea  wamekuwa na tabia ya kugawana vijana ili  kuwasaidia katika kampeni na mwisho wa siku  wamekuwa  wakikigawa  chama  jambo ambalo ni hatari zaidi  katika uimarishaji  wa chama .

Pia Msowoya  aliwataka  vijana kujiandaa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya serikali za mitaa ili ikiwezekana mitaa mingi zaidi mwakani katika mkoa  wa Iringa  kuongozwa na vijana .
 
Aliwaagiza viongozi wa UVCCM kwa ngazo zote kutoa taarifa ya kuwepo kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi, ambao wanataka kuitumia jumuiya yao kama njia ya mafanikio yao kiuongozi.

“UVCCM ya sasa haitakubali kuyumbishwa wala kugawanywa na mtu yeyote mwenye nia ya kuomba madaraka, itafanya kazi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” alisema Msowoya.

Akizungumzia uchaguzi wa chipukizi mkoani humo, Katibu wa UVCCM mkoani humo Alawi Haidar alisema umefanyika kwa amani na utulivu na kwamba, watoto hao wameweza kuwapata viongozi bora walioona wanawafaa.

Mwenyekiti  mpya wa chipukizi  mkoa Enock Meshack  Luhala mbali ya kuwashukuru  wajumbe  waliomchagua bado  alisema kuwa ataendelea  kutoa  ushirikiano mkubwa kwa chama ili kuhakikisha chama kinapata  ushindi  wa kishindo katika mkoa  wa Iringa .

 Akitangaza matokeo hayo, Haidar alisema Mwenyekiti mpya wa chipukizi mkoani humo, Enock Luhala alifanikiwa kushindwa kwa kura 18 kati ya 33 zilizopigwa na kuwashinda wenzake, Ashraf Mpogole aliyepata kura 12 na Magreth Lusingo kura nne.

Katika nafasi ya mkutano mkuu wa chipukizi taifa, Junior Mlelwa alishinda kwa kura 26 na kuwabwaga wenzake, Halid Aziz na Christopher Dalu.


Wengine walioshinda ni Tausi Mgambo, Rukia Kimweli na Amina Kimweli kuwa wajumbe wa kamati ya uendeshaji mkoa.

No comments:

Post a Comment