Tuesday, November 12, 2013

VIJANA MKOANI KILIMANJARO WAHIMIZWA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MILENIA

IMG_3534
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungmza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro juu ya umuhimu wa kujihusisha na kazi za Umoja wa Mataifa wakati wa ziara za kutembelea shule mbalimbali za mkoa huo.
Na. Mwandishi wetu.
Vijana wa shule za sekondari nchini wameaswa kuwa mabalozi wazuri pindi watakapomaliza masomo yao juu ya kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya milenia kwa sababu ni dira ya maendelo ya taifa na dunia kwa ujumla.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho, Lyamungo na Umbwe sekondari hivi karibuni, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema malengo ya milenia yanagusa Nyanja zote za maendelo kwa vijana walio na wasio mashuleni.
Bi. Nkhoma amewataka wanafunzi wafanye kazi za kujitolea na kuhakikisha wanapeleka elimu waliopata kupitia vilabu vya Umoja wa Mataifa kwa jamii na kuhamasisha dhana ya kujitolea kwa maslahi ya nchi.
“kila ndani ya saa moja tuna vijana 50 ambao wanapata maambukizi ya VVU kati ya miaka 14-24 ambao wengi kati ya hao ni Wasichana, hivyo msijihusishe na masuala ya mapenzi mnapokuwa mashuleni”, amesema Bi. Nkhoma.
IMG_3558
Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha takwimu za Mimba za Utotoni zilizotolewa hivi karibuni (“Young People Today. Time to Act Now”) ambapo asilimia 25 ya watoto wa kike chini ya miaka 14 wanapata wakiwa mashuleni.
IMG_3550
Pichani juu na chini ni vijana wa shule ya Sekondari Umbwe wakifuatilia kwa umakini mjadala wa masuala ya Umoja wa Mataifa uliiongozwa na Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
IMG_3544
IMG_3574
Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser akifafanua jambo kwa vijana waliojiunga na klabu za Umoja wa Mataifa shuleni hapo juu ya umuhimu wa kuwa na cheti cha klabu ya Umoja wa Mataifa
IMG_3586
Msafara wa wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakitazama baadhi ya kazi mbalimbali zinazofanywa na klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya sekondari Umbwe ikiwemo shughuli za kuchangia damu, kusafisha mazingira na mengineyo yajihusishayo moja kwa moja na shughuli za jamii.
IMG_3630
"Ubovu wa miundombinu ni changamoto kubwa kwa ziara yetu lakini ujumbe wa shughuli za Umoja wa Mataifa lazima ziwafikie walengwa".
IMG_3679
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifurahia uwepo wake mbele ya wanafunzi wa Kibosho Girls shule ambayo binafsi alisoma miaka 20 iliyopita, ambapo pia ujio wake ulikuwa chachu na hamasa kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
IMG_3666
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkhoma Ledama.
IMG_3692
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwasisitizia wasichana wa shule ya Kibosho juu ya umuhimu wa kujiamini na kujitambua wakati wa maamuzi yao binafsi.
IMG_3738
Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa.
Kwa picha zaidi ingia hapa

No comments:

Post a Comment