Wednesday, November 20, 2013

TFM YATOA SOMO KWA WANAHABARI WA MITANDAO ,YASISITIZA UMAKINI NA UBORA WA HABARI ZA UCHUNGUZI

Mwezeshaji wa mafunzo ya uboreshaji wa uandishi katika mitandao ya kijamii (blogu) kutoka mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) Simon Mkina katikati akimsikiliza kwa makini mwezeshaji mwezake Beda Msimbe wakati akitoa mfano wa uandishi bora wa habari za mitandaoni.

 Raziah Quallatein Mwawanga kutoka  TFM  akijitambulisha  mbele  ya  washiriki  wa mafunzo  ya ubora  wa uandishi  katika  mitandao  ya kijamii
 Mkufunzi  kutoka  Jamii Forums akiwanoa  wanahabari  juu ya uandishi  bora  wa mitandaoni 

Na  Francis Godwin Blogu-Dodoma


MFUKO  wa  vyombo  vya habari  Tanzania (TMF)  umewataka  wanahabari nchini  kujikita  zaidi  katika  uandishi wa habari za  uchunguzi ili  kuisaidia  jamii na  Taifa  badala ya  kuendelea  kuandika  habari  zisizo na uchunguzi. 


Rai hiyo  imetolewa leo  na mwezeshaji  wa  warsha  ya  siku nne  ya uboreshaji  wa uandishi  katika mitandao  ya  kijamii zikiwemo Blogu Bw. Simon Mkina  wakati wa mafunzo  hayo mjini  Dodoma.


Bw  Mkina alisema  kuwa  pamoja na TMF  kuamua  kuanza  kutoa  ruzuku   ya  habari  kwa blogu ila  bado sehemu  kubwa ya  wanahabari nchini   wamekuwa  wakiripoti matukio  zaidi  badala ya  kufanya uchunguzi na kuandika habari za kichunguzi  ambazo  ndizo zenye    msaada mkubwa katika Taifa.

Kwani  alisema kuwa  uandishi  ambao  utaleta  mabadiliko katika vyombo vya habari  hasa mitandao  ya  kijamii ni pamoja  na kuwa na ukweli wa  kutosha  wa habari zinazoandikwa badala ya  kutumia  vyombo  hivyo  kuandika habari  zisizo  na maadili pamoja na habari  zinazohatarisha usalama  wa taifa .


Hata  hivyo alisema  kuwa  hivi  sasa  mitandao  ya kijamii imekuwa  ikitumia  vibaya  japo  wanahabari   wamiliki  wa mitandao hiyo  watajipanga na  kujiunga na uandishi wa habari za kiuchunguzi  na zinazozingatia  maadili upo  uwezekano mkubwa  wa TFM  kuendelea  kutoa  ushirikiano kwa kutoa ruzuku kwa mitandao  hiyo ya kijamii.

Pia  alisema  kuwa wanahabari  hao   20  ambao  wamepatiwa mafunzo  ya  uandishi  bora  wa blogu ni chachu  kwao kutumia  mafunzio hayo kuleta  mabadiliko ya kweli kwa mitandao  hiyo ya kijamii ili iwe mfano mzuri  kwa vyombo  hivyo  vya habari za mtandaoni.


Katika  hatua  nyingi  Mkina alitaka  wanahabari hao  na  wengine ambao  hawajapatiwa mafunzo ya  uboreshaji  wa habari za mkitandaoni ni  vema  sasa  kurejea katika maadili .


Huku mkufunzi  wa mafunzo hayo  Beda Msimbe  alisema  kuwa lengo la kuanzisha mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza  kufanyika ni  kutoka kuongeza ubora  wa uandishi  unaozingatia maadili katika mitandao  hiyo .

Alisema  kuwa  Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF)  umeanza  kutoa mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza na  kuwa  washiriki wa mafunzo hayo ndio  ambao  watapatiwa  ruzuku ya kwanza ya kufanya kazi  ya uandishi  kulingana na mawazo  ya habari  watakayowasilisha .


Pia  aliwaonya   wanahabari hao  kuacha  kutumiwa na wanasiasa   na badala  yake  kukubali kutumiwa na  wananchi  zaidi ili  kuwasaidia katika  kufikisha matatizo  yao kwa  viongozi  wao.


Msimbe  alisema  kuwa usalama  wa wanahabari  utaendelea  kuwa hatarini iwapo  wanahabari hawataheshimu maadili  na kuendelea  kutumika kwa  kuchafua  ama  kufanya uandishi  usio  zingatia maadili.


 Kwa  upande  wake afisa miradi wa TMF  Japheth Sanga  aliwataka  wanahabari hao  mbali ya kuandika habari za uchunguzi kuhakikisha  wanaheshimu sheria za nchi .

Kwa  upande wake  

Pia  alisema  TMF imekuwa ikisaidia  vyombo vya habari na  wanahabari nchini hivyo ili wanahabari hao kuendelea kunufaika na vema  kujiunga kama kundi na kuomba fedha  zaidi TMF.


Alisema iwapo  watafanya  vema katika awamu hii ya kwanza  wao kama TMF wataendelea  kuwasaidia na ikiwezekano kutoa vifaa vya kufanyia kazi wanahabari hao.

No comments:

Post a Comment