Friday, November 15, 2013

SPIKA ANNE MAKINDA ASHIRIKI MKUTANO WA WABUNGE UMOJA WA MATAIFA


 Mhe. Anne Makinda ( Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   akiwa katika mkutano wa mwaka unaowakutanisha maspika na wabunge kutoka  nchi mbalimbali  duniani katika mkutano wa siku mbili  unaofanyika  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Mkutano  huu umeandaliwa kwa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Inter-Parliamentary Union ( IPU) katika  mkutano huu pamoja na mambo mengine wabunge wanajadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu nafasi wa  mabunge katika  majadilianao yannayoendelea  hivi sasa kuhusu ajenda mpaya  za Maendeleo Endelevu baada ya  2015.  Kulia kwa Mhe. Spika ni   Balozi  Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum

Maspika wa Mabunge na wabunge kutoka  zaidi ya nchi mia moja jana alhamis, wameanza mkutano wao wa mwaka wa siku mbili unaofanyika  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  jijini New York, Marekani.

Ujumbe wa  Tanzania katika  mkutano  huo, ambao  umeandaliwa kwa ushirikiano  baina  ya   Umoja wa Mataifa kupitia Baraza lake la Uchumi na Maendeleo ( ECOSOC) na Inter- Parliamentary Union ( IPU)   unaongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Anne Makinda (Mb).

Mada kuu ya  mkutano huu ni  Re-thinking sustainable development: the quest for a ‘ transformational’ global agenda in 2015 ambapo  wabunge wamekuwa wakijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mchango wa Mabunge katika  maandalizi ya   Malengo  Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015.

Mkutano umefunguliwa na  Rais wa Baraza  Kuu la  Umoja wa  Mataifa,  Bw. John Ashe ambaye  alitambua mchango wa  mabunge na wabunge katika kusimamia siyo tu utendaji wa serikali, utungaji wa sheria na sera mbalimbali na ukusanyaji wa mapato  bali pia katika  kuhakikisha ustawi na maendeleo ya wananchi. Akiwahimiza kuchagiza na kuhimiza  maandalizi  ya   ajenda  mpya za malengo mapya ya maendeleo endelevu.

Wengine waliozungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano ni  Rais wa ECOSOC Bw  Nestor Osorio na Rais wa IPU Bw. Abdelwahadi Radi

Aidha wabunge  katika siku ya  kwanza ya mkutano wao    pia wamejadiliana na kubasilishana mawazo na  uzoefu   katika mada inayohusu ‘ Jinsia kama kitovu  cha maendeleo,namna ya kuunda  malengo mapya’.   Mkazo ukiwa katika kuhimiza ushiriki wa wanawake,  vijana na asasi za kiraia

Katika siku ya pili ya mkutano  utakofanyika siku ya ijumaa,  Mhe, Spika  Anne Makinda ( Mb) atakuwa  mmoja wa wanajopo katika mada itakayokuwa inazungumzia  utawala wa kidemokrasia na nafasi yake katika  Maendeleo endelevu.


Washiriki wengine katika  jopo hilo watakuwa ni  pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa Bw. Jan Eliasson, Balozi wa  Usiswi katika  Umoja wa Mataifa,  Bw. Paul Seger na Balozi wa Costa  Rica, Bw. Eduardo Ulibarri.



No comments:

Post a Comment