Tuesday, November 26, 2013

Rais Kikwete awaasa vijana kujituma kufanya kazi katika warsha ya Fursa jijini Dar leo

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.Mh. Rais ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha hiyo.Picha zote na Othman Michuzi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa,Ahmed Lussasi akizunguma katika Warsha ya Fursa namba alivyo
Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasseb Abdul a.k.a Diamond akitoa ushuhuda wake wa namna alivyoanza na mpaka alipofikia sasa,ambapo ameweza kuiona Fursa na kuweza kugawana fursha hiyo na vijana wenzake anaofanya nao kazi kila siku.Kushoto ni Mwanafursa Mwingine,ambaye pia ni Msanii wa Mashairi,Mrisho Mpoto.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatma Ally akielezea namna alivyoipata Fursa kwa kupitia Ufugaji wa Nyuki.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasikiliza vijana mbali mbali walopata Fursa na kuweza kufanikiwa katika maisha yao.
Mrisho Mpoto akizungumzia Fursa yake.

Wadau mbalimbali wa Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu wakimsikiliza kwa makini Mwenyeshaji wa Kampeni hiyo ya Fursa,Ruge Mutahaba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akiwapongeza vijana walioiona Fursa.
Wadau mbali mbali wakiwa kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment