Imeelezwa kuwa ufaulu wa mtihani
wa kumaliza darasa la
saba kwa mwaka 2013 umepanda kwa masomo yote kwa asilimia
19.89 ikilinganishwa na ilivyokuwa kwa mwaka uliopita.
Kwamba, wakati mwaka jana wahitimu waliopata asilimia
100 walikuwa asilimia
30.72, mwaka huu wameongezeka kuwa
asilimia 50.61. Pia, somo ambalo
watahiniwa hao wamefaulu
zaidi katika mtihani wao ni Kiswahili ambapo
ufaulu ni
asilimia
69.06 huku wakiwa wamefeli zaidi kwenye somo la
Hisabati ambalo ufaulu upo
chini kwa asilimia 28.62.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA),
Dk. Charles
Msonde alisema wanafunzi 427,606
walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi
mwaka
2013 huku kiwango cha udanganyifu kikizidi kudhibitiwa
hivyo kupungua.
Alisema NECTA imefuta matokeo yote ya mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi kwa
watahiniwa 13, ambao walibainika
kufanya udanganyifu kwenye mtihani au kurudia
pasipo ruhusa
ya Baraza. Watahiniwa waliofutiwa mwaka jana ni 293. Alisema kati ya wanafunzi hao, 844,938 waliofanya mtihani
huo wamepata alama
zaidi ya 100 katika alama 250:
“Idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61. Kati
yao wasichana
walikuwa 208,227 (sawa na asilimia 46.68) na wavulana 219,379
sawa na asilimia 55.01,” alisema.
Dk. Msonde alisema katika ufanyaji wa mtihani huo,
pia walikuwepo watu wenye
ulemavu, ambapo wasichana
walikuwa 219 na wavulana 257.
Alisema matokeo hayo yatapelekwa maeneo yote husika
ili mchakato wa upangaji
shule ukifanyika kwa watahiniwa
wote waliofaulu mtihani huo wa kumaliza elimu
ya msingi.
Kuhusu usahihishaji mitihani, Dk. Msonde alisema ili kujiridhisha
na usahihi wa
zoezi la usahihishaji wa kutumia mfumo wa kompyuta
(Optical Mark Reader - OMR),
sampuli za karatasi 20,795 za
majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya
48
zilichukuliwa kutoka shule za mikoa tisa ya (Iringa, Kagera,
Shinyanga,
Manyara, Njombe, Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga)
na kusahihishwa kwa mkono: “Ulinganifu
baina ya alama
za watahiniwa zilizopatikana kwa kusahihishwa kwa
mkono na zile
zilizotokana na usahihishaji wa mfumo wa
kompyuta ulifanyika na kubaini
kompyuta ilikuwa sahihi,”alisema.
Amesema makosa yaliyojitokeza katika karatasi zilizosahihishwa
kwa mkono ni
kuweka pata pale ambapo kuna kosa ama kuweka
kosa pale ambapo kuna pata, makosa
ambayo kwenye usahihishaji
wa kutumia kompyuta hakuwepo.
Matokeo ya dalasa la saba yaliyopachikwa hapo juu pia
yanapatikana katika
tovuti za:
|
No comments:
Post a Comment