Saturday, November 2, 2013

Maelfu wajitokeza Gulio la Vodacom Mlimani City

Mkuu wa kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akizungumza na waandishi wa Habari, wakati Gulio la mauzo ya bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu kwa wateja wake iliyofanywa na kampuni hiyo katika viwanja vya makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar e s Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango kwa wateja wake.
Mamia ya wateja waliojitokeza katika Gulio "Vodacom Expo" lililofanyika katika viwanja vya makao makuu ya ofisi hizo Mlimani City jijini Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza kampuni hiyo ilifanya Gulio hilo kwa kuuza bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango kwa wateja wake.
Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika Gulio la  mauzo ya bidhaa yaliyofanyika katika viwanja vya  Makao makuu ya Vodacom yaliyoko mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya bidhaa zimeuzwa kwa bei ya chini ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa wateja wake.

Akizungumzia juu ya Gulio hilo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa alisema, amefurahishwa na mwitikio wa wateja wa wakazi wa Dar es Salaam ambao  wamejitokeza kwa wingi katika siku hiyo huku akitanabaisha kuwa siku zote kampuni yake imekuwa mstari wa mbele kutoa huduma bora kwa wateja wake.

"Ninawapongeza sana wakazi wa Dra es Salaam amabao wamejitokeza kwa wingi katika maonesho haya tumeona namna ambvavyo wanaendelea kutuunga mkono,  juu mnada huu kuwa watajipatia bidhaa hizi zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu, tulicho amua kukifanya ni kuwawezesha wateja wetu kununua bidhaa ambazo wamekuwa wakiziota kila siku kuzinunua kwa bei nafuu," alisema Twisaa na kuongeza kuwa.

"Sambamba na maonesho hayo pia kulikuwa na michezo ya watoto na chakula, hivyo wazazi wanaweza kuja pamoja na familia zao.
Twissa aliongeza kuwa "Ni kwa mara ya kwanza mnada huu mkubwa kufanyika nchini Tanzania, dhumuni ni  kuwawezesha wateja wetu kujipatia simu na vifaa vingine vya umeme kwa gharama nafuu na zenye punguzo la hali ya juu tofauti na zinavyouzwa madukani.

"Tuliona ni vema kuwawezesha wateja wetu  na wale wasioweza kumudu gharama za moja kwa moja madukani ambazo zinakuwa ni bei ya juu tofauti na tutakavyo uza siku hiyo.

Mauzo na manunuzi ya bidhaa hizo yatafanyika papo kwa hapo siku ya mnada ambapo wateja wataweza kununua kwa fedha taslimu au kupitia njia ya M - PESA.

Maonesho hayo yataambatana si tu na mauzo ya bidhaa hizo pia kutakuwepo na chakula na michezo na burudani mbalimbali ambapo watu watakuwa wakijumuika pamoja. Ni siku nzuri kwa familia kujumuika pamoja, marafiki kukutana na kubadilishana mawazo na vilevile kujenga urafiki mpya wenye manufaa kwa wote.

Baadhi ya bidhaa ambazo zinauzwa siku ya mnada huo ni kama vile; Apple Ipad 2-64GB, Apple Ipad 2-32GB, Apple Ipad 2-16GB, Samsung Tablet 10.1, ZTE V9 Tablet, BB Playbook 64GB, BB Playbook 32GB, ZTE MF68-Mobile TV, Blackberry 9320, Blacberry 9630, Blackberry 9105, Samsung P520-GSM, Samsung i9003 Galaxy, Samsung i780-GSM, Nokia N97, Sony Ericson Experia, Huawei Phone-V720, Samsung N 150, Desktop Phone G201, K3805 HSDPA Data Car, K3565 HSDPA Data Car, K3570 HSDPA Data Car, Antenna for Router B, Sandisk SD 1GB, PHONE BATTERY 225, Charger V125 & V225, ZTE-Web Box, Router:E5331-Pocket na nyinginezo nyingi.

Mnada huo utafanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo yaani kuanzia tarehe 2 na 3 ya siku za Jumamosi na Jumapili za mwezi huu wa Novemba mwaka huu katika moja ya ukumbi wa makao makuu ya Vodacom Tanzania yalilyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment