Monday, October 28, 2013

sharjah yaahidi kusaidia kunyanyua uchumi mkoa wa lindi

Picha ya ramani ya kiwanda kitakavyokuwa ikikamilika kazi ya Ujenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Meis Merey Ally Saleh akimpokea Dr Rashid aliyetembelea kukagua kazi za ujenzi wa kiwanda cha saruji mjini Lindi.
Mhandisi Rashid wa Sharjah alievaa kilemba akiangalia mchoro wa ujenzi alipokuwa akikaua eneo la Ujenzi ambapo Mkurugenzi wa Meis na Meneja wake wakitolea maelezo.
majengo na kazi inavyoendelea ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Na Abdulaziz Lindi

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari ya Nchi ya Sharjah UAE, Mhandisi Rashid Al Leem amefurahishwa na hatua ya Kampuni ya Meis kuanza kwa kasi ujenzi wa kiwanda cha saruji katika wilaya ya Lindi huku akiutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza juhudi ili kukamilisha kwa wakati kama ilivyokusudiwa ili mji huo uongeze ajira hali itakayosaidia kuinua Uchumi. 

Alibainisha hayo alipokuwa akiongea na globu hii muda mfupi baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua Ujenzi wa Kiwanda hicho alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea wilaya hiyo baada ya kukutana na Serikali ya Zanzibar ambapo aliahidi Kuwekeza katika nyanja mbalimbali.

Dr Rashid alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kuongeza kiwango cha ajira, kipato cha wananchi wa kawaida wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa jumla na kupunguza gharama za ujenzi wa makazi kwa kupata saruji kwa bei ya chini na kwa ukaribu kuliko ilivyo sasa.

“Kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hiki itakuwa ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mikoa ya kusini kupata saruji kwa bei nafuu na ajira kwa vijana wa mikoa hii ambapo Nchi yetu imeamua kutaka kuwekeza ndio maana pia nitatembelea Bandari ya Mtwara.

Kwa upande wake meneja wa mradi huo, Valerian Magembe alisema ujenzi wa kiwanda hicho umefikia hatua mzuri kwani mitambo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 25 kutoka nchini China inatarajiwa kuwasili hivi karibuni baada ya kupakilwa huko shanghai,

“Mitambo inayotarajia kuwasili ni mitambo mizito yenye cbm 6200 ya kusaga mawe,kunyangia, kutenganisha, pamoja kuweka dawa,kuumua na kuunda simenti na kwa sasa tayari imepakiwa kwenye meli toka Shaghahi, China na ipo safarini itawasili muda wowote kuanzia sasa ”alisema Magembe.

Aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uko kwenye hatua ya kusaga mawe baada ya kufanya kazi kubwa ya kukata mlima ili kufanya eneo hilo liwe tambarale.

“Kazi kwenye eneo ilikuwa ngumu kwani lina miinuko mikubwa hata hivyo sehemu kubwa tumeikamilisha na tupo hatua za mwisho”alibainisha Magembe.

Aidha ujezi wa kiwanda cha sementi Lindi ulinza mwezi februari mwaka 2013 na unatarajia kukamilika septemba 214 na kuajiri watu zaidi 2000 pamoja na kuzalisha tani 20000 kwa siku na kuongeza kipato kwa wakazi wa mkoa wa Lindi.

Katika ziara hiyo Dr Rashid aliongoza ujumbe toka Serikali ya Sharjah huku akiwemo Balozi wa Comoro Nchini Balozi Islam Ally Saleh ambapo pia msafara ulitembelea makazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa,Bernard Membe kijijini Rondo wilayani humo

No comments:

Post a Comment