Wednesday, October 2, 2013

Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF waanza rasmi leo jijini Arusha

Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 2 mpaka Oktoba 5,2013.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Lulu Mengele akifafanua jambo juu ya Muonekano wa Logo Mpya ya Mfuko huo iliyozinduliwa Rasmi leo kwenye Ukumbu wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa kuitika kwao wito kwenye Mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 2 mpaka Oktoba 5,2013.

Kijana Peter William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachama na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachama na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili kupoteza maisha.
Ilikuwa ni huzuni tu wakati vijana hao wakitoa ushuhuda wao wa namna walivyoweza kusaidiwa kimasomo na Mfuko wa Pensheni wa PPF pindi walipoondokewa na wazazi wao.
Waheshimiwa Wabunge wakifatilia kwa umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua.
 Viongozi kutoka Chama cha Wafanyakazi.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbali mbali ndani ya Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifatilia mkutano huo.
 Sehemu ya Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini.
 Wajumbe wa Bodi ya PPF.
 Wadau wa PPF wakijadiliana jambo.
 Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa Tuzo wa Washindi mbali mbali wa PPF wanaoongoza kwa kuwasilisha michango yao kwa wakati. 
 Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo Mpya ya PPF iliyoambatana na Tovuti Mpya ya PPF.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio.
 Hivi ndivyo inavyoonekana Nembo Mpya ya PPF. 
 Nembo na Tovuti.
 Mrisho Mpoto akitoa burudani. 
Muonekano wa Nembo mpya.
 Burudani ya Ngoma za asili. 
 Wadau wakiwa Mkutanoni. 

No comments:

Post a Comment