Saturday, October 19, 2013

MEYA SILAA AJA NA KAMPENI KABAMBE YA KUCHANGIA MADAWATI KUPITIA SANAA

DSC_0429
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kuhusu kampeni ya ‘Dawati ni Elimu’ kupitia wasanii mbalimbali wa kuchora nchini. Kulia kwake ni Msanii Robin Mtila na Kushoto ni Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha na Mustafa Hassanali Mratibu wa Kampeni hiyo.
DSC_0446
Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha akizungumzia mchango wa hoteli yake katika kampeni ya Dawati ni Elimu yenye kauli mbiu ya "Kalisha mmoja boresha Elimu".
DSC_0457
Mchoraji Robin Mtila akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake ambapo ameelezea umuhimu wa sekta ya Elimu katika fani ya sanaa nchini.
DSC_0497
Mkurugenzi wa Advert Construction Ltd Dhmy Jog akizungumza na waandishi wa habari baada ya kampuni yake kuchangia Tsh 10 milioni kwenye kampeni hiyo ya kuondoa tatizo la madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.
DSC_0463
Baadhi wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha kubwa la Sanaa lenye lengo la kuchangia kampeni ya Dawati ni Elimu.
DSC_0466
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
DSC_0534
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Sanaa ya Uchoraji pamoja na baadhi ya wadhamini wa kampeni hiyo. .Kampeni ya Dawati ni Elimu yakusanya Tsh 1bilioni mpaka sasa lengo ni kufikia Tsh 4.98bilioni .atoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha la mwaka dawati ni elimu

Na Moblog Team
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa akishirikiana na Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel na wasanii kumi maarufu nchini wameandaa tamasha kubwa la sanaa la mwaka kwa wasanii wa kuchora (Painters) lenye lengo la kuchangia kampeni ya “Dawati ni Elimu” katika shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam. 

Moblog linaripoti Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mhe Silaa amesema kuwa katika kampeni hiyo ya ‘Dawati ni Elimu’ kupitia programu ya (Annual Mayors Charity Ball) wameamua tarehe 16 ya mwezi Novemba kuwa na tamasha la sanaa ya uchoraji itakayowashirikisha wasanii kumi maarufu nchini.

“kwenye tamasha la tarehe 16 mwezi Novemba mwaka huu wasanii wa kuchora wataweza kuchora picha mbalimbali kwa ubunifu wao na kuweza kuonyesha kazi zao pamoja na kuuza kwa wateja katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel na sehemu ya mapato yatachangia madawati na asilimia zingine itakuwa faida yao baada ya mauzo kwenye maonyesho ya picha ,” amesema.

Amesema kuwa katika tamasha hilo la sanaa ya kuchora wasanii wataweza kuonyesha kazi zao za sanaa katika harakati za kuhamasisha jamii kuchangia kupunguza tatizo la madawati kwenye shule za msingi na sekondari kupitia kauli mbiu ya “Kalisha mmoja, boresha elimu”

Silaa aliongeza pia kwamba katika tamasha hilo la mwaka pia kutakuwa na chakula cha mchana kwa wageni wote wataohudhuria Shughuli hiyo ambayo itakuwa ya wiki nzima katika kuhakikisha lengo hilo la kupata madawati kwenye shule linafanikiwa. Amesema kuwa kwa sasa takwimu zinaonyesha asilimia 30 ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanakaa chini kwa kukosa madawati katika shule nyingi za kata mkoa wa Dar es Salaam.

Alisisitiza kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala wanatafuta njia bora ambayo wachangiaji wanaweza kuchangia kupitia mitandao ya simu ili kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa hiyo adhimu na pesa za wananchi zinafanya kazi iliyokusudiwa.

“watanzania ni lazima waamke ili waweze kuchangia maendeleo ya elimu nchini katika kusukuma mbele maslahi mapana ya nchi kwa siku za usoni ili taifa letu liweze kuwa na wananchi waliopata elimu bora na si bora elimu,” alisisitiza Mhe Silaa .Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha amesema kuwa ni sehemu ya mpango wa hoteli hiyo kurudisha faida wanayopata kwenye jamii ili kusaidia kupunguza matatizo na changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu.

“Ni muhimu kwa wafanyabiashara kushirikiana na jamii inayoitumikia na tutaendelea kusaidia jamii katika siku za usoni tukiwa kama sehemu ya jamii husika,’ amesema.

Naye Mkurugenzi wa Advert Construction Ltd Dhmv Jog amesema kampuni yake inatambua umuhimu wa sekta ya elimu kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla katika kufuta ujinga.

Amesema kampuni yake kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii kimetoa Tsh 10milioni katika kusaidia kampeni hii ya “Dawati ni Elimu” ili kupunguza na kuondoa kabisa tatizo la madawati mashuleni Wasanii wataopata nafasi ya kuonyesha kazi zao za sanaa ya kuchora ni Robin Mtila, Aggrey Mwasha, Salum Kambi, Cathbert Mkocha, Haji Chilonga, Tobias Miza, James Haule na Victor Malulu.

No comments:

Post a Comment