Sunday, October 6, 2013

MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA LUTHER BAGAMOYO YAFANA

Baadhi ya wanafunzi kati ya 45 wanaosoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakimkabidhi zawadi ya kumshukuru mwalimu wao Mkuu Mtanga Gerson wakati wa Mahafali yao ya kwanza ya Kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 wanategemea kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha Nne hivi karibuni.Wapili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Rasmali Watu Mary Ngonyani,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo na Mkurugenzi wa shule hiyo Aumsuri Kiwelu.
Mtaalamu wa kutengeneza maabara za shule ,(Lab Technical) na mwalimu wa masomo ya Chemistry, Biology katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Luther iliyopo eneo la Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bw.Kalistus Mwendapole akimuonesha Mkurugenzi Rasmali Watu Mary Ngonyani,alipotembelea maabara ya shule hiyo akiwa mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 wanategemea kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha Nne hivi karibuni.
Mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani Mkurugenzi Rasilimali watu wa Dawasa Bi.Mary Ngonyani,akimkabidhi Cheti Anna Kiwali aliefanya vizuri katika masomo ya Hesabati na Sayansi wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Wanaoshuhudia, Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Dr.Aumsuri Kiwelu na Mkuu wa shule hiyo Mtanga Gerson.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Luther wakivishana mashada wakati wa mahafali yao ya kwanza ya kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2010 jumla ya wanafunzi 45 walisherehekea mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani Mkurugenzi Rasilimali watu wa Dawasa Bi.Mary Ngonyani ,akimkabidhi Cheti Zainabu Chungu wakati wa mahafari hiyo wanaoshuhudia (wapili kutoka kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa shule hiyo Anna Kiwelu na Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Dr.Aumsuri Kiwelu.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa pwani wakifurahia jambo wakati wa Mahafali yao ya kwanza ya kidato cha Nne iliyofanyika shuleni hapo.
Mlezi wa wa wanafuzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo ,Constansia Masawe akiwasalimia wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliofika katika sherehe ya mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne kwa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzii wa kitato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo wakiwa katika mahafali yao ya kwanza tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 walihitimu.
Kaimu Mkurugenzi wa Shule ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Anna Kiwelu akiongea wakati wa Mahafari ya kwanza ya shule hiyo . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Dawasa Mary Ngonyani , Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Dr.Aumsuri Kiwelu .Mahafari hayo ya kwanza yamewajumuisha jumla ya wanafunzi 45. Ambao wanategemea kufanya mitihani ya kidato cha Nne hivi karibuni.
Protoko Ofisa wa Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani,John Mwakilya akiwapa utaratibu baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Nne katika mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2010.Jumla ya wanafunzi 45 wa kidato cha Nne wanategemea kufanya mtihani wa taifa hivi karibu.

No comments:

Post a Comment