Tuesday, October 29, 2013

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA PILI WA BOHARI YA DAWA (MSD)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Charles Pallangyo akizindua mpango mkakati wa pili wa bohari ya dawa MSD unao tarajiwa kuanza julai 2014 hadi juni 2020 wenye lengo la kuongeza ubora kiutendaji katika uzinduzi uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam jana.
Kamimu Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa (MSD) Bw. Cosmas Mwaifwani akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika uzinduzi huo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Charles Pallangyo akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI Bw Deo Mtasiwa mara baada ya kuzindua mpango huo jana katikati ni Kamimu Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa (MSD) Bw. Cosmas Mwaifwani.
Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bw. Charles Pallangyo akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa mbalimbali mara baada ya uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

MAFANIKIO ya kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nchini ni matokeo ya kuisha kwa mkakati wa kwanza ulianza julai mosi 2007 na kumalizika Juni 30 mwaka huu imefahamika.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Charles Pallangyo Dar es Salaam jana, wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kujadilimpango mkakati wa pili bohari ya dawa MSD unao tarajiwa kuanza julai 2014 hadi juni 2020 wenye lengo la kuongeza ubora kiutendaji ,kutoa huduma na kukuza mtaji wa bohari ya dawa.

 ” Mpango mkakati wa kwanza ulileta mafanikio makubwa kwa kupunguza upungufu wa dawa nchini  na kupanuka kwa maghala katika makao makuu na ofisi za kanda” alisema Pallangyo.

Aliongezea kuwa mpango mpya 2014-2015 unatarajia kutekeleza malengo mbalimbali yakiwemo kuongeza imani kwa wateja, kupunguza gharama na kuboresha mazingira ya kazi.

Katika hatua nyingine MSD, wameweka malengo katika mpango mkakati ambayo ni kuongeza upatikanaji wa dawa kwa silimia 95 , kuongeza upatikana kwa huduma kwa wateja kwa asilimia 100, kuongezeka kwa soko kwa asilimia 80, kuanzisha secta binafsi katika uzalishaji wa dawa ndani na nje ya nchi na kuboresha mahusiano na wadau kwa asilimia 95.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa MSD, Idris Mtulia alisema kuwa bohari ya dawa inampango wa maendeleo unaolenga  kuboresha na kuleta ufanisi  katika utendaji kazi ambayo hupangwa kila baada kipindi fulani.

Mtulia aliongezea kuwa, mpango mkakati wa pili umetayarishwa kwa kutumia mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi unaojulikana kama mfumo mizania, una lengo la kusimamia, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa mpango Mkakati ili kuhakikisha huduma hiyo inafika kila pembe ya nchi yetu.

No comments:

Post a Comment