Thursday, September 19, 2013

WAZIRI MKUU AZINDUA MFUMO WA UFATILIKI WA ASALI YA TANZANIA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Ukwekezaji, Dr. Mary Nagu akikata utepe kuzindua Mfumo wa Ufatiliki (Traceability System) wa Asali ya Tanzania, Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anayeangalia kushoto kwa Waziri Nagu ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Elibariki Mmari na kushoto kwake ni Fatma Kange, Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania.
 Mgeni Rasmi akiwa na wageni wengine  wakifatilia uwasilishwaji wa mfumo huo uliokuwa ukifanywa na afisa wa GS1 Tanzania.
 Wakuu wa Wilaya na Wabunge wakifuatilia uzinduzi huo,
 
 Maofisa watendaji wakuu toka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makani uwasilishwaji wa mfumo huo.
 
 Wadau wa nyuki toka mikoa husika wakifuatilia kwa makini.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange akitoa maelezo ya awali kuhusiana na mpango mzima wa Mfumo wa Ufatiliki wa Asali.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi akiuliza swali wakati wa kongamano baada ya uzinduzi.
 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwakaribisha wadau wa Asali shambani kwake Zuzu Mkoani Dodoma, Mwenye Kaunda suti nyeupe ni Mh. Suleiman Kumchaya Mkuu wa Wilaya Tabora aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwasa.
 Zuzu Shambani kwa Waziri Mkuu.
 
 Sehemu ya mabanda ya kufugia nyuki kwa njia ya kisasa

 Hapa mambo mswano kwa nyuki





  Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na wadau wa Asali shambani kwake Zuzu Mkoani Dodoma, 

Mtaalamu wa Mifumo ya Ufatiliki toka GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti akitoa mada ya mfumo mzima kwa wadau.

No comments:

Post a Comment