Tuesday, September 3, 2013

TGNP WAJIPANGA KUMKOMBOA MWANAMKE WA PEMBEZONI KUSHIKA MADARAKA

 Wanaharakati  wa  mtandao  wa kijinsia  Tanzania  (TGNP)  wakiwa katika maandamano  ya  miaka 11 ya  tamasha la TGNP nchini na maadhimisho ya miaka 20  ya harakati  za ukombozi wa mwanamke
Na  Francis Godwin Blog
WANAHARAKATI  wa mtandao   wa  jinsia  Tanzania (TGNP) wamefanya maandamano makubwa  ya kuazimisha  miaka 20 katika  kupinga  vitendo  vya ufisadi pamoja na ukandamizaji  wa  wanawake .

Huku mtandao  huo ukidai  kuwa  umejipanga  kuendeleza  mapambano  ili  kuwawezesha  wanawake  wa pembezoni  kuchukua  madaraka  ya  uongozi katika chaguzi  mbali mbali ili  kusaidia  kuwakomboa  wananchi  wa  pembezoni .

Mkurugenzi  mtendaji  wa  TGNP Usu  Mallya  alitoa kauli hiyo  leo   katika tamasha  la 11 la TGNP linaloendelea  katika viwanja  vya TGNP Mabibo  jijini Dar es Salaam.

 “Tunashuhudia  uporaji  wa  maliasili  zetu  yakiwemo  madini  katika maeneo  yetu

…sasa  tunataka  kuona Raslimali  za  Taifa  ziwanufaishe  wananchi   kwa kuzingatia   usawa  wa  kijinsia”

Alisema  lazima  wanawake  na jamii  nzima  kupambana  kuleta  mabadiliko ya  kweli ya  mwanamke na mwanaume  pamoja na  watoto huku  wakitazamwa  zaidi wale  waliopo pembezoni .

“….Uchambuzi  wetu  unaonyesha  kuwa  wanaozidi kubebeshwa  mizigo mikubwa zaidi ni wanawake  waliopo pembezoni ambao  TGNP  na  washirika  wengine  tumejipanga  kuendelea kuwapigania  ili nao  waweze  kufaidi matunda  ya  Taifa…

,hivyo  lengo  letu  kuwawezesha  wanawake  wa  pembezoni  kuchukua madaraka ili kuweza  kuwakomboa  wanawake  nchini “

Tumefanikiwa  topasa  sauti  kwa  kipindi  cha  miaka  20  sasa   katika  kupinga  vitendo  vya ufisadi pamoja na ukandamizaji  wa  wanawake .

Aidha alisema  kuwa harakati  ambazo TGNP na  washirika  wengine  wamekuwa  wakizifanya  ni zimelenga  kulikomboa  bara  la Afrika  ,kulikomboa  Taifa na  kukomboa  raslimali    za  taifa  zisiwanufaishe  watu  wachache .

Kwani  alisema  kuwa  TGNP wameanza  kupasa  sauti  katika  kuhakikisha  huduma  za  jamii  zinapatikana kwa  watu wote na  kuepuka  mfumo dume na kandamizi kwa  wanawake na  watoto toka  mtandao  huo  ulipoanzishwa  mwaka 1993.

Alisema  miaka 20 iliyopita Suala  la jinsia  lilikuwa ni kama hadhithi  na suala la mfumo  dume  lilikuwa  halizungumzwi kabisa  ila  kwa  sasa  kila mmoja anatambua na  kuzungumzia  suala  hilo masuala ya jinsia na mfumo  dume .

Kuhusu  kuendelea  kukithiri  kwa  rushwa  za  ngono katika maeneo ya kazi  Mallya  alisema kuwa rushwa  ya  ngono ni chanzo  cha  kuendelea  kumnyanyasa  mtoto  wa  kike  nchini na  kuwa  bado  suala  hilo ni kikwazo na wao kama  wanaharakati  wataendelea  kupaza  sauti na kupambana na vitendo  vya  rushwa za  ngono .

“Bajeti  ya  kijinsia lazima  iweze  kuanzishwa  ili  kuwezesha  haki na usawa  kati ya  wanaume na  wanawake  inakuwepo  kama njia ya  kuyawezesha makundi  yote  kunufaika na raslimali  ya  Taifa “.

Wakati  huo huo  washiriki  wa  maandamano  na tamasha  hilo  wameitaka  serikali  kuchukua hatua  kali kuwawajibisha  wale  wote  wanaoendesha  biashara  ya madawa  ya  kulevya  ambayo yameendelea kulichafua  Taifa na hata  kuwafanya  vijana  wengi  kupoteza maisha kwa utumiaji wa madawa  hayo na kuacha mateso kwa  wanawake na watoto.

No comments:

Post a Comment