Wednesday, September 11, 2013

NYUMBA YA ASHA BARAKA YATEMBEZEWA NYUNDOZZZ ENEO LA HANANASIFU JIJINI DAR

 Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.

Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.

Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.

Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili kuendelea na biashara.

Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.

Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.

Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.

Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
 Katapila likiendelea kubomoa....
 Asha Baraka akisimama mbele ya Frem zake eneo hilo kuwazuia jamaa hao kuendelea na zoezi hilo hadi upatikane muafaka na wahusika kwanza.
 Asha Baraka, akionyesha alama ya pili iliyowekwa jana na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo.....
 Wananchi wakimsikiliza Asha Baraka.....
 Sehemu ya madimbwi yaliyoachwa na wachimbaji hao mara ya kwanza ambayo kwa sasaa yameanza kukauka.
 Nyumba ya Asha Baraka (kushoto) inayotakiwa kubomolewa na (kulia) ndiyo Ghorofa lilalokwepwa ili kupindisha barabara hiyo jambo linalofanya kubomolewa kwa nyumba za upande mmoja.
 Asha Baraka, akionyesha alama za awali zilizowekwa kwa rangi nyekundu ambazo zinaonyesha kuwa hadi ukuta wa ghorofa unatakiwa kuondoka...
 Alama hiyo ipo kwenye kibanda hiki cha mkaa ambacho kipo sambamba na ghorofa hilo..
 Alama iliypchorwa kwa mkaa mara ya pili jana.......
Sehemu ya uhalibifu uliotokea jana wakati wa zoezi hilo.....katika moja ya fremu zilizopo eneo hilo...

3 comments:

  1. Hapa zinahitajika taarifa zaidi ili comments zitolewe kwa usahihi.

    ReplyDelete
  2. Good morning,

    Jamani Tanzania jaribu kutumiya usitarabu sasa unapo muharibiya mwezako hivyo hujui hiyo pesa alipataje labda bado hajalipa deni so do unapo zidisha mashaka kwa mwenzako.

    ReplyDelete
  3. Naishauri Serikali na mamlaka zake kwa ujumla wajaribu kufanya mambo kwa mipango sio kukurupuka na kutumia mabavu inaleta picha mbaya sna mbele ya jamii na kusababisha wananchi waichukie serikari na viongozi wake bila sababu ya msingi na tukiendelea kufanya mambo bila usimamizi makini tunajenga Taifa lenye chuki zidi ya watawala kitu ambacho ni hatari sana kwa mustakbali wa Taifa letu.Tujaribu kuweka mikakati ya maendeleo ya maeneo yetu hususani miundo mbinu kwa mitaa ya jiji letu kwa kuweka mipango ya muda mrefu na kuwahi kuzuia maeneo yte ambayo yapo kwenye mipango ya upanuzi wa barabara kuliko kufanya kazi kwa zima moto. Tujenge taifa la wananchi wenye kupenda nchi yao ili waweze kuilinda na kuipigania kwa lolote kuliko hivi sasa wananchi wanaonekana kama hawana haki yoyote ktk nchi hii hususani watu wa chini ila walionacho hata wakiua leo kesho wapo nje kwa dhamana ila mwizi wa kuku anahukumiwa miaka kadhaa jela wakati mhujumu uchumi wa Taifa anachekewa na kuwa nje kwa dhamana.

    ReplyDelete