Saturday, September 28, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AZURU JIMBO LA NEBRASKA NCHINI MAREKANI,

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe Ricketts kwenye uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens, 7, mara baada ya Mama Salma kutua kwenye uwanja wa ndege wa Omaha  katika jimbo la Nebraska nchini Marekani
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyeshwa na Bwana James Ricketts, Rais na Mtendaji Mkuu wa  wa Taasisi ya Oppoturnity Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya elimu kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi  hiyo yenye Makao Makuu yake huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani 
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Opportunity Education iliyoko huko Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo kwa kutambua mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake ya WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina mama..
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Taasisi ya Opportunies Education kwenye ofisi za taasisi hiyo huko Omaha Nebraska nchini Marekani. Kulia kwake ni katubu wa WAMA Bw. Daudi Nasibu
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Mshauri Mwandamizi wa   United Nations Fund for International Partnership (UNFIP) 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akwia  kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Mshauri Mwandamizi wa   United Nations Fund for International Partnership (UNFIP) 
 .Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Dr. Marjorie Kastelnik, Dean, College of Education and Human Sciences kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska ambapo Mama Salma alishiriki kwenye Gala to support Global Education kwenye Chuo Kikuu cha Lincoln huko Nebraska
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Bwana Joe Ricketts kwenye hafla ya Taasisi ya Support Global Education .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa waliohudhuria hafla ya Taasisi ya Support Global Education iliyoandaliwa kwa ajili ya kumtunuku tuzo maalum Bwana Joe Ricketts kwa juhudi zake za kuboresha elimu duniani hasa katika nchi zinazoendelea. 
PICHA NA JOHN LUKUWI

Taasisi ya Opportunity Education kutoa tablets kwa wanafunzi nchini

Na Anna Nkinda – Maelezo, Lincoln
28/9/2013 Taasisi ya fursa ya  Elimu (Opportunity Education) ya nchini Marekani imeazimia kuanzisha mradi wa  laptop ndogo (tablets computer) kuanzia mwezi Januari mwaka 2014 nchini ambazo zitatumika kufundishia ili walimu waweze kufundisha haraka na kwa ufanisi zaidi pia wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza  zaidi.
Hayo yamesemwa jana  na Joe Ricketts ambaye ni mwanzilishi na mtendaji mkuu wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuchangia uugwaji mkono wa utoaji elimu barani Afrika iliyoandaliwa na taasisi ya Malaika  ya nchini humo na kufanyika katika  chuo Kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln .
Ricketts alisema mradi huo kwa mara ya kwanza utaanzia nchini Tanzania ambapo wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule 10 tofauti watapewa laptop ndogo kwa ajili ya kusomea na baada ya kipindi cha mwaka mmoja watafanya  mtihani ili kuangalia tofauti iliyopo kwa wale waliokuwa wakitumia na wasiotumia.
Baada ya majaribio hayo kama kutakuwa na mafanikio basi mradi huo utasambazwa katika shule nyingine nchini Tanzania ili kila mwanafunzi aweze kupata nafasi ya kusoma kwa kutumia laptop  hizo na hii itakuwa ni nafasi kwao ya kuweza kujitunza zaidi.
“Kwa mara ya kwanza nilipokuwa nchini Tanzania nilipita  Serengeti na kukuta  mtu  anajitahidi  kutengeneza nyumba ambayo ni ngumu kuitengeneza hii inamaana kuwa mwalimu mmoja alikuwa anafundisha wanafunzi zaidi ya miamoja niliamua kuanzisha mahusiano na shule hiyo ambayo niliwapelekea vifaa mbalimbali vya kufundishia”.
“Lengo la  kuanzishwa kwa Taasisi hii ni kutoa msaada wa kielimu ikiwa na nia ya kufanya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea ili wale wanaotoka katika familia maskini waweze kusoma na kupata ajira pale watakapokuwa wamemaliza masomo yao na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha”, alisema Ricketts.
Alimalizia kwa kusema kuwa program zao za kufundishia wanafunzi zimeandaliwa kwa lugha ya kiingreza lakini hivi sasa wameanza kuandaa program hizo kwa njia ya Kiswahili jambo ambalo litazifanya shule ambazo zinafundisha kwa lugha hiyo nazo kunufaika na Taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia  kuboresha elimu nchini na kuiomba kuangalia uwezekano wa kuzifikia  shule, walimu  na wanafunzi waliopo vijijini ambao nao wanahitaji kupata njenzo nzuri za kufundishia na material mazuri ya kusoma kama ilivyo kwa wanafunzi wa mjini.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeeo (WAMA) alisema kuwa kupitia taasisi hiyo ameweza kuwasaidia watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao hawakupata nafasi ya kupata elimu kuwapatia ufadhili wa masomo na hivyo kuendelea na masomo yao.
Pia ameweza kuinua uchumi wa wanawake jambo ambalo limewafanya waweze kuimarisha hali zao za maisha kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kuwaongezea mitaji ya vikundi vyao vya maendeleo.
Mama Kikwete alisema, “Nakupongeza Bwana Ricketts kwa kazi unayoifanya ya kuzisaidia shule zaidi ya 400 nchini Tanzania msaada unaoutoa wa vifaa vya kufundishia unawafanya walimu waweze kufundisha masomo yao vizuri naamini tutajenga mahusiano mazuri kati ya Taasisi yako na WAMA ili kuhakikisha kuwa program hii inafanikiwa na kutimiza malengo yake”.
Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa nchini mwaka 2006 walianza kufanya kazi na shule moja ya msingi na hadi kufikia sasa  shule 434 zikiwemo za Sekondari 33 zimenufaika kwa kupata vitabu, DVD na zana za kufundishia.
Kwa upande wa shule za sekondari wanatoa mwongozo wa mwalimu ambao unamuongoza kirahisi jinsi ya kuwafundisha wanafunzi , laptop ambazo zinamasomo yaliyorekodiwa ambayo ni ya sayansi, hesabu, kiingereza na maarifa ya jamii ,projecta na Televisheni ambazo zinasaidia kuonyesha masomo na vitabu na video inawasaidia wanafunzi kujifunza somo la kiingereza kwa njia ya kusikiliza na kusoma.

Mama Kikwete alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya Taasisi hiyo yaliyopo  katika mji wa Omaha na kujionea nyenzo mbalimbali za kufundishia vikiwemo vitabu na  DVD  zikiwa zimefungwa kwa ajili ya kupelekwa katika nchi mbalimbali zinazoendelea za bara la Afrika na Asia ikiwemo Tanzania.

No comments:

Post a Comment