Friday, September 13, 2013

KINANA: SHINYANGA KUNEEMEKA NA VIWANDA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa Kambarage huku akishuhudiwa na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqinq.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwa baiskeli kutoka Uwanja wa Kambarage kuelekea uwanja wa Shycom kwenye mkutano wa hadhara.
 Balozi wa China nchini Dk.Lu Youqinq akiwapungia wananchi wakati akielekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shycom,Shinyanga mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa China nchini wakiwasubiri wenzao tayari kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
 Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Balozi wa China nchini na Mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa na wa kihistoria ulifanyika leo tarehe 13 Septemba 2013.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa Shycom na baiskeli tayari kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto),Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqinq na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye , Balozi wa China alipata fursa ya kuelezea kwa wananchi wa Shinyanga namna uwekezaji utaweza kuunufaisha mkoa huo ambapo viwanda vya nguo, kusindika mafuta, asali na bidhaa zitokanazo na mifugo vinategemewa kujengwa katika mkuo huo na kutoa nafasi kwa ajira ,kuinua uchumi ,elimu na kuondoa kabisa umasikini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyiaka kwenye uwanja wa Shycom mkoani Shinyanga.
 Mbunge wa Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia yeye anachofanya ni kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na kwake maendeleo kwa wana Shinyanga ndio kitu cha msingi.
 MNEC wa Wilaya ya Shinyanga mjini Ndugu Gasper Kileo akihutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom,mkoani Shinyanga leo.
 Mbunge wa Viti maalum kupitia UWT Shinyanga Ndugu Lucy Mayenga akiwahutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu alikuwa anahitimisha ziara yake mkoani hapo.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwasalimu wakazi wa Shinyanga mjini wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini  ambapo aliwaasa wananchi waepuke 'makanjanja wa siasa' na badala yake washirikiane na viongozi wao katika kuleta maendeleo.
 Umati wa watu uliofurika wakati wa mkutano wa mwisho wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Shycom.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisoma vijiji vitavyofaidika na mradi wa umeme vijijini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom leo tarehe 13 Septemba 2013.
 Mbunge wa Kishapu akiruka kwa furaha baada ya kusikia vijiji vya wilaya yake vitafaidika na mradi wa umeme wa vijiji.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu pikipiki mpya watakazopewa makatibu kata wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiondoka uwanja wa Shycom baada ya kumaliza mkutano wenye mafanikio makubwa kwa wakazi wa Shinyanga kwani walipata fursa ya kutambua namna mkoa wao utakavyobadilika ndani ya miaka 10 ijayo kwani wawekezaji wa kutoka China wameanza kuwekeza viwanda amabavyo vitatoa ajira za kutosha, kuinua uchumi kwa wakulima na pia kutoa elimu ya kilimo na teknolojia.

No comments:

Post a Comment