Sunday, September 8, 2013

JK AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI WA MAGU

 Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jaqueline Liana, (kushoto,) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (katikati) mara baada ya kuwasiri katika makao makuu ya kata ya Lugeye ambako kulitolewa taarifa ya wilaya ya Magu
 Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma ya wananchi wa kabila la Wasukuma wanayocheza na nyoka aina ya chatu wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye iliyopo wilayani Magu. Zahanati hiyo imegharimu kiasi cha  milioni 170.
 Wananchi wakishuhudia Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu t
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi jengo la zahanati ya Kata ya Lugeye huko wilayani Magu t
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Shadrack Faustino Mbilizi aliyehudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye huko Magu na pia alipokea kupokea kadi yake ya kitambulisho cha matibabu kwa wazee .
 Rais Jakaya Kikwete akipokea kitambulisho cha matibabu kwa wazee kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jaqueline Liana kwa ajili ya kupewa Kanali Mstaafu Shadrack Mbilizi na mkewe Mariam Said wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la zahanati ya Lugeye
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wa kata ya Lugeye wakati wa sherehe za kufungua jengo la zahanati ya kata hiy
  Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu eneo la  Ilungu karibu na mji wa Magu.  Jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 6 na milioni 700 litakapokamilika. 
 Rais  Jakaya Kikwete ngoma ya utamaduni wilaya ya Magu kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu
Rais  Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Magu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu. Picha zote na John Lukuwi

No comments:

Post a Comment