Wednesday, September 18, 2013

CHUO KIKUU BAGAMOYO KUWANOA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kozi mpya ya kuwanoa watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojulikana kwa jina la ‘Akiba Uhaki’, iliyofanyika Kawe Beach jijini Dar es Salaam juzi. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila, Mkuu wa kitivo cha Sheria cha Chuo hicho, Dk. Natujwa Mvungi na Mratibu wa Programu ya taasisi ya Akiba Uhaki, Kepta Ombati.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika hafla uzinduzi wa kozi mpya ya watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Afrika Mashariki.
 Baadhi ya wadau wakiwa katika hafla hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo hicho, Dk. Natujwa Mvungi (kuli) na Mratibu wa Programu ya taasisi ya Akiba Uhaki, Kepta Ombati. (kushoto).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Costa Mahalu (kulia),wa pili kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho, Dk. Sengondo Mvungi, mwanafunzi wa chuio hicho, Hapiness Katabazi na mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Salum Mkambala.

 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akipeana mkono na mwanafunzi kutoka Kenya, Daniel Otieno.  
Muziki ulichukua nafasi yake.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akimpongeza mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Jane Kacuculi kutoka Uganda, ambaye amepata udhamini wa kusoma katika Chuo hicho kutoka katika taasisi ya kiraia ya Haki Uhaki ya nchini Kenya.

 DAR ES SALAAM, Tanzania

SERIKALI imekipongeza Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), kwa uamuzi wake wa kuanzisha kozi ya kuwanoa watu wanaojitambulisha kuwa wao ni watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwasababu kozi hiyo itasaidia watetezi wa haki za binadamu kufahamu wanachokifanya katika jamii.

Hayo yalisemwa juzi usiku na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila kwaniaba ya Mkuu wa Pwani, Mwantumu Mahiza katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika chuo kikuu cha Bagamoyo Kawe Beach jiiini Dar es Salaam, wakati akizindua rasmi program hiyo ya mafunzo ambayo imepewa jina la’ Akiba uhaki’ ambapo inakuwa ni ya kwanza kutolewa hapa nchini.

Sila alisema programu hiyo inaendeshwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) na kufadhiliwa taasisi ya kiraia ya Haki Uhaki yenye makao makuu yake nchini Kenya, tayari imeishapata wanafunzi kumi toka nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi na kwamba masomo hayo yatakuwa yakitolewa kwa miezi sita na kuwataka wale wote wanaojiita wanaharakati hapa nchini wafike katika chuo hicho ili waweze kufundishwa kwanza jinsi ya kufahamu haki za binadamu ni zipi, na haki za kijamii ni zipi na hao wanadamu wanatakiwa wazitii sheria za nchi wakati wakizidai hizo haki zao bila shuruti.

“Tumeona katika mataifa ya wenzetu vurugu kila kukicha na hata hapa nchini kuna baadhi ya watu wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitumia kinga hiyo kupotosha ukweli wa mambo ambayo yanafanywa na serikali zao kwa kisingizio kuwa wa ni watetezi wa haki za binadamu wakati hata elimu ya kutetea hizo haki za binadamu hawana …leo serikali inapenda kupongeza program hii kwani itasaidia sana kuondoa mivutano na malumbano baina ya watetezi wa haki za binadamu na serikali kwani mtu atakayepata elimu hii atakuwa ameelimika na kufahamu haki za binadamu zinapaswa zidaiwe kwa kutumia amani”alisema Sila.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Profesa Costa Ricky Mahalu aliishukuru serikali kwa kukubali kuja kuzindua program hiyo kwani programu ni yakwanza kutolewa katika vyuo vya hapa nchini na program hiyo itawezesha kuondoa malumbano baina ya serikali na watetezi wa haki za binadamu kwani ni wazi hivi sasa kumeibuka watu wanaojitambulisha kuwa ni watetezi wa haki za binadamu wakati hawana hata elimu ya huo utetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitoa baadhi ya matamko ambayo hayana mantiki katika suala zima la utetezi wa haki za binadamu hali ambayo alisema ikiachwa iendelee italeta madhara katika jamii.

“UB inaamini katika elimu zaidi…hivyo UB imeona ni jambo jema kuanzisha program hiyo ya mafunzo ya muda mfupi kwa wale wote wanaotaka na wanajiita watetezi wa haki za binadamu waje kufundishwa masuala hayo na  waadhiri waliobobea katika eneo hilo la masuala ya haki za binadamu”alisema Profesa Mahalu.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dk. Natujwa Mvungi ambayo program hiyo ya Akiba uhaki inatolewa chini ya kitivo chake alisema jumla ya wanafunzi 10 toka katika nchi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki wa kozi ya Akiba Uhaki ,wameishafika hapa nchini na wanaanza mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita kuanzia wiki hii chuo hapo na kwamba wanafunzi hao wamefadhiliwa ada ya kusoma kozi hiyo na taasisi isiyo ya kiserikali yenye makao makuu yake nchini Kenya ya Akiba uhaki na kuwataka wale wote wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu wakati hawana elimu ya kuonyesha wamefudhu kozi hiyo,wasisite kuja kupata elimu hiyo chuo hapo.

No comments:

Post a Comment