Monday, September 9, 2013

Arusha yaigaragaza Kagera 3-0 katika fainali za taifa za U-15 za Copa Coca-Cola 2013

 Beki wa timu ya Kirimanjaro Jamens Geofrey (katikati) akiwatoka wachezaji wa  mbeya Yusuf Honroli (kushoto) na  Jackson Mwaibambe katika mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Selemani Mwalimu akiwania mpira na mshambuliaji wa Mbeya Hamfrey Nyeo  katika mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0. 
 Beki wa timu ya Mbeya Emmanuel Ntindi (kulia) akipiga hesabu za kumtoka mchezaji wa  Kilimanjaro James Geofrey katika mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0. 
Mshambuliaji  wa  timu Mbeya Yusuf  Honroli  (kushoto) akimtoka beki wa Kilimanjaro Simon Soka  katika mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0.

 Kiungo wa  timu ya Mbeya Emmanuel Ernest ( katikati) akitoa pasi huku walinzi wa Kilimanjaro Bernld Temba (kulia) na  James Geofrey wakijiandaa kumzuia katika mechi ya fainali za Copa Coca-Cola Taifa kwenye Uwanja wa Karume leo. Kilimanjaro walishinda 1-0.


 Mshambuliaji wa timu ya  Mbeya,Yusuf Honroli (kushoto) akiwania mpira na mabeki wa Kilimanjaro,Abidal Ramadhani (kulia) na Simon Soka  katika mashindano ya Copa Cocacola kwenye Uwanja wa Karume 
 Timu ya Copa Coca-Cola ikiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kukwea pipa kuelekea Afrika Kusini kwenye kambi ya mafunzo ya soka yakishirikisha timu za vijana kutoka barani Afrika. Anayehojiwa ni Afisa Habari wa Coca Cola Tanzania Gerald Ndalahwa
Timu ya Arusha  imeigaragaza timu ya Kagera 3-0 katika  mchezo wa fainali za taifa za  vijana chini ya umri wa  miaka 15 za Copa Coca-Cola 2013 katika uwanja wa Tanganyika packers , Kawe jijini Dar es Salaam  . Mpaka wanaenda mapumziko kagera walikua wanaongoza 2-0
Arusha walionyesha kuwazidi wapinzani wao kila idara ,kwa kucheza kandanda safi na kupata goli la kwanza katika dakika ya pili kupitia kwa Mohamed Said ambaye alikuwa mwiba katika ngome ya Kagera. Goli la pili lilipachikwa na mshambulia hatari Bakari Athanas katika dakika ya 27.
Katika kipindi cha pili Kagera walifanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la wapinzani wao lakini bila mafanikio.  Baada ya hapo timu ya Arusha ilifanya mashambulizi mengi langoni mwa wa pinzani wao na kufanikiwa kupata goli la tatu katika dakika ya 56 kupitia tena kwa Mohamedi Saidi.
Katika mechi nyingine ya Copa Coca-Cola iliochezwa  jana iliwakutanisha Kilimanjaro na Mbeya katika uwanja wa kumbukumbu wa Karume ambapo Kilimankaro waliibuka na ushindi wa 1-0 , goli lililofungwa na Selemani Mwalimu katika dakika ya kwanza baaada Kilimanjaro kufanya  shambulio la ghafla.
Washiriki wapya katika michuano hii ya Copa Coca-Cola timu ya Geita ilijikuta katika wakati mgumu sana baada ya kukubali kipigo cha 4-1 kutoka kwa watoto wa mjini Temeke katika uwanja wa Tumbi , Kibaha ambao walitoka sare ya 1-1 dhidi ya wapinzani wao timu ya Ilala katika mechi ya ufunguzi iliofanyika jumapili katika  uwanja wa kumbukumbu wa Karume jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika  ufunguzi  huo Makamu wa pili wa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ramadhani Nasib , alisema kuwa mashindano ya vijana ni msingi wa kuibua vipaji vya wachezaji ambavyo vitaleta mabadiliko katika medani ya soka nchini.
Kwa upande wake Meneja bidhaa wa Coca-Cola nchini Maurice Njowoka  alisema kuwa Coca-Cola itaendelea kudhamini mashindano ya vijana kuanzia ngazi ya wilaya mpaka taifa.
Alisema kuwa  kubadilisha mashindano kutoka umri wa miaka 17 mpaka 15 ni moja kati ya juhudi za Coca-Cola pamoja na TFF na FIFA ili kuwafikia vijana wadogo wakike na wakiume ilikukuza vipaji vyao.
Wakati huo huo timu ya Copa Coca-Cola imeondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwenye mafunzo ya wiki moja siku ya jumapili. Mafunzo hayo yatawapa uzoefu vijana hao katika kuendeleza vipaji vyao.

Mafunzo hayo yatawakutanisha timu kutoka nchi mbaimbali katika bara la  Afrika. 

No comments:

Post a Comment