Monday, August 26, 2013

WANANCHI WA WILAYA YA BAGAMOYO MKOANI PWANI WATOA MAONI KUHUSU RASIIMU YA KATIBA MPYA

 Mratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Hidaya Mohammed akiongea katika mkutano wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo  mwishoni mwa juma. Wengine kulia ni Wajumbe wa Tume hiyo Bw. Omar Sheha, Dkt. Salim Ahmed Salim na Alhaji Said El-Maamry.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza Mratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Hidaya Mohammed  (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa majadiliano mjini humo
 Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mzee Omary Yahaya Mhando akitoa maoni yake katika mkutano wa Baraza hilo
 Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Jumanne Chiboko akitoa maoni yake kuhusu rasimu ya katiba wakati wajumbe hao waliojigawa katika makundi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Omar Sheha (kushoto) akiongea na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo (kulia) ambao wataongoza majadiliano ya makundi kabla ya kuanza kwa majadiliano kuhusu rasimu ya katiba. Picha na tume ya katiba

No comments:

Post a Comment