Monday, August 19, 2013

TANAPA YAFUNGA RASMI AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UJANGILI KWA UHARAKA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akikagua gwaride la Kikundi cha Kukabiliana na Uhalifu kwa Haraka (Rapid Response Team) kilichohitimu mafunzo yao katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mwishoni mwa wiki.
Wahitimu wa RRT wakiapa Kiapo cha Utii mbele ya Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.
Wahifadhi wakifuatilia kwa makini zoezi la uhitimishwaji wa mafunzo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Ruaha Dk. Christopher Timbuka, John Shemnkunde, Mtango Mtahiko na Godwell Meing’ataki.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Martin Loibooki akisoma maelezo kuhusu mafunzo hayo kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akiongea na wahitimu.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Martin Loibooki (kulia) akiwa na Kamanda Venance Tossi.
Wahitimu wakionyesha zoezi la kumsogelea adui wakiwa tayari kwa lolote.
Mashambulizi yanaendelea baada ya adui kuonekana huku vumbi la risasi likionekana kwa mbali.
Picha ya pamoja ya wahitimu na Mgeni Rasmi.
Makamanda wa Vita dhidi ya Ujangili walioendesha mafunzo haya. Kutoka kulia ni Genes Shayo, Venance Tossi na mtaalamu kutoka Afrika Kusini Martin Mthembu. Picha zote na Mdau Pascal Shelutete wa TANAPA

No comments:

Post a Comment