Tuesday, August 27, 2013

NSSF YAWAAGA WAJUMBE WA BODI NA KUWAKARISH​A WAPYA


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Wajumbe wa Bodi iliyomaliza muda wake na kuikaribisha bodi mpya katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
Meneja Kiongozi, Uhusiano, Huduma kwa Wateja wa NSSF ,Eunice Chiume akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau baada ya kutoa hotuba yake.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF iliyomaliza muda wake, Hildegard Mziray akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa NSSF. 
 Meneja Kiongozi,uhusiano huduma kwa wateja wa NSSFEunice Chiume  (kulia) akiwa makini wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau alipokuwa akizungumza. 
 Mwenyeki wa bodi ya NSSF, Abubakar Rajab (kati) akifurahia jambo 

Ofisa Uhusiano Kiongozi wa NSSF, Juma Kintu akizungumza wakati wa hafla hiyo. 

 Mwenyetiki wa Bodi, Abubakar Rajabu akiwaongoza wajumbe wa bodi ya NSSF kupata chakula cha jioni. 
 Wajumbe wakiendelea kupata chakula. 
 Meneja Kiongozi,uhusiano huduma kwa wateja wa NSSF ,Eunice Chiume  akipata chakula.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akimkabidhi zawadi Mwenyetiki wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajabu.
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF iliyomaliza muda wake, Hirdegard Mziray akipokea zawadi yake kutoka kwa Dk. Dau.
 Baadhi ya wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao wakipokea zawadi zao.

 Picha ya paamoja.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akiwa na Makamu Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Zuhura Muro na Meneja Kiongozi,uhusiano huduma kwa wateja wa NSSFEunice 
Chiume  (kulia) 

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewapongeza Wajumbe wa Bodi ya shirika hilo waliomaliza muda wake, kwa utendaji bora uliotukuka licha ya changamoto kubwa walizokabiliana nazo katika kipindi chao madarakani.
Pongezi hizo zilitolewa jana usiku na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau, wakati wa chakula cha usiku cha kuiaga bodi hiyo chini ya Uenyekiti wa Aboubakar Rajab na kuikaribisha bodi mpya, ambayo Mwenyekiti huyo ataendelea na wadhifa wake.
Dk. Dau alisema kuwa, ingawa kuagana ni furaha, lakini tukio hilo pia ni huzuni kwa uongozi na wafanyakazi wa NSSF, kutokana na aina ya utendaji na ushirikiano wa bodi hiyo na Menejimenti ya shirika hilo tangu mwaka 2010 ilipoingia madarakani.
“Menejimenti ya NSSF, inatambua na kujivunia ushirikiano uliokuwapo baina yake na bodi hii tunayoiaga leo. Ilifanya kazi kwa weledi na hadi inamaliza muda wake hatukuwahi kufikishana bungeni, wizarani wala kutupiana lawama,” alisema Dk. Dau.
Aliongeza kuwa, NSSF inajivunia mafanikio na hatua mbalimbali za mchango wa Bodi hiyo katika shughuli za Ustawi wa Jamii, ikiwamo ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Daraja la Kigamboni na Barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze.
Aliongeza kuwa, anaamini bodi mpya itamalizia masuala hayo na mengine mbalimbali yaliyoanzishwa na bodi hiyo, ukiwamo mchakato wa uanzishwaji wa Tawi la Hospitali ya Apollo ya India hapa nchini, ili kuwezesha wanachama wa NSSF kutibiwa hapa.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi iliyoagwa, Hildegard Mziray, alisema kwa niaba ya bodi hiyo anapenda kuishukuru menejimenti na wafanyakazi wa shirika hilo kwa ushirikiano, lakini pia kujali na kuthamini mchango wao.
Aliitakia kila la kheri Bodi mpya katika kipindi chao cha miaka mitatu na kuitaka ichukulie mema na mazuri yaliyofanywa na bodi yake kama changamoto, katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo endelevu ya shirika hilo.

No comments:

Post a Comment