Sunday, August 18, 2013

MSHINDI WA NYUMBA YA AIRTEL YATOSHA AKABIDHIWA UFUNGUO WA NYUMBA,WENGI IRINGA WAIMWAGIA SIFA AIRTEL WAPANIA KUJIUNGA SASA


 Madereva  boda  boda wakiwa  tayari  kuelekea  nyumbani kwa mshindi wa  nyumba eneo la Frelimo mjini Iringa leo
 Safari  ya  kuelekea  Frelimo ikianza  


 Hakika  Airtel Yatosha  wengi kujiunga na Airtel 



Madereva  wa  boda  boda  mjini  Iringa  wakitoka maeneo ya  Frelimo mjini  Iringa wakati wa  ziara  ya wafanyakazi  wa Airtel makao  makuu na Iringa  kumtembelea mshindi  wa  nyumba  ya  kwanza  ya Airtel Yatosha  Bw Sylivanus Juma Wanga  ambae  ni mhasibu wa taasisi  isiyo ya  kiserikali ya TARWOC ambae amekabidhiwa fungu ya nyumba  na kuelekea  jijini Dar es Salaam kukabidhiwa nyumba yake

 Mshindi  wa nyumba ya Airtel Yatosha  Bw Sylivanus Wanga  kulia akimpokea kwa  furaha ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando baada ya  kumtembelea  mtaani kwake Frelimo Iringa 


Mshindi  wa nyumba  ya kwanza  ya Airtel Bw Bw Sylivanus Juma Wanga   na  ndugu  zake wakifurahia  kutembelewa na  wafanyakazi  wa kampuni ya simu ya Airtel nyumbani kwao Frelimo mjini Iringa kwa  ajili ya  kukabidhiwa funguo na hati ya  nyumba  yao kabla  ya kuelekea  Dar es Salaam kukabidhiwa  nyumba yake  kulia wa kwanza ni ofisa mahusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando, meneja  wa  Airtel nyanda za  juu kusini Beda Kinunda ,mke  wa mshindi Bi Veronica Wanga ,Bw Sylivanus Wanga na shemeji  yake Bi Martha Kibiki

 Ofisa  mahusiano  wa Airtel Bw  Jackson Mmbando (kushoto) na meneja wa Airtel mikoa ya  kusini Beda Kinunda wakiwa  nje ya  nyumba ya mshindi  wa nyumba ya kwanza ya Airtel yatosha eneo la Frelimo mjini Iringa



 Ofisa habari wa Airtel Bw  Jackson Mmbando wa  pili  kulia akizungumza lengo la ziara yao mjini Iringa kwa mshindi  wa nyumba  ya kwanza ya Airtel Yatosha nyumbani kwake  Frelimo Iringa  
 Mmoja kati  ya  wafanyakazi  wa taasisi ya TARWOC Bw  Beni Kibiki akiwa nyumbani kwa mshindi wa nyumba ya  kwanza  ya  Airtel  Yatosha  leo eneo la Frelimo mjini Iringa



Mshindi  wa nyumba  ya kwanza  ya Airtel Bw Bw Sylivanus Juma Wanga   na  ndugu  zake wakifurahia  kutembelewa na  wafanyakazi  wa kampuni ya simu ya Airtel nyumbani kwao Frelimo mjini Iringa kwa  ajili ya  kukabidhiwa funguo na hati ya  nyumba  yao kabla  ya kuelekea  Dar es Salaam kukabidhiwa  nyumba yake  kulia wa kwanza ni ofisa mahusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando, meneja  wa  Airtel nyanda za  juu kusini Beda Kinunda ,mke  wa mshindi Bi Veronica Wanga ,Bw Sylivanus Wanga na shemeji  yake Bi Martha Kibiki

 Hii  ndio  nyumba anayoishi  mshindi  wa  nyumba  ya Airtel Yatosha iliyopo  eneo la Frelimo mjini Iringa
 Meneja  wa Airtel yatosha  mikoa ya  kusini Beda Kinunda  akiogoza familia ya mshindi  wa Nyumba kuelekea  ukumbini  katika hafla ya  kukabidhiwa funguo na hati ya  nyumba kabla ya  kuelekea  jijini Dar es Salaam  kukabidhiwa  nyumba yake

 Eneo la Frelimo  mjini Iringa ambalo mshindi  wa nyumba ya kwanza  ya Airtel yatosha anaishi
 Wafanyakazi  wa Airtel  wakiwa nje ya  gari  wakimsubiri mshindi wa nyumba  kushuka 
 Mke  wa mshindi  wa  nyumba ya Airtel Yatosha  Bi  Veronica Wanga akishuka katika  gari tayari kwenda  ukumbini  kukabidhiwa  funguo na hati  yao
 Mshindi  wa  nyumba wa  pili  kushoto akiwa ameshuka katika  gari  tayari  kuelekea  ukumbini
 Wafanyakazi  wenzake na mshindi  wa nyumba  kutoka taasisi ya  TARWOC 

 Baadhi ya  wafanyakazi  wenzake  na  wananchi  waliofika  kushuhudia tukio hilo  wakianza  kujiounga na shindano hilo



 Ofisa  mahusiano  wa Airtel Bw Jackson Mmbando  akionyesha funguo ya  nyumba aliyoshinda Bw Sylivanus Juma  Wanga (kushoto) kulia ni meneja wa Airtel mikoa ya  kusini 

 Ofisa  mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akimpongeza mshindi wa nyumba ya kwanza kati ya nyumba tatu zinazoshindaniwa Bw Sylivanus Juma  Wanga kushoto huku meneja  wa Airtel mikoa ya  kusini Beda Kinunda  akishuhudia


Meneja  wa Airtel mikoa ya  kusini Beda Kinunda  akimkabidhi funguo ya nyumba mshindi wa  nyumba ya kwanza  ya Airtel Yatosha  jana  kutoka Frelim mjini Iringa Bw Sylivanus Juma Wanga  wanaoshuhudia  ni mke wa mshindi Bi Veronica  Wanga na ofisa mahusiano  wa Airtel Bw Jackson Mmbando


Ofisa  mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akizungumza na familia ya mshindi  wa nyumba ya Airtel yatosha  jana nyumbani kwa mshindi huyo eneo la Frelimo mjini Iringa  jana kutoka kushoto ni meneja  wa Airtel nyanda za juu kusini Beda Kinunda mshindi  huyo wa nyumba Bw Sylivanus Juma Wanga  na mkewe Bi Veronica Wanga

 Mmbando  akitoa ufafanuzi juu ya mshindi  huyo alivyopatikana kabla ya  kumkabidhi hati yake  ya nyumba  leo
 Ofisa mahusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando  akionyesha  hati ya  nyumba 

 Mshindi  wa  nyumba ya  Airtel yatosha  akisoma hati ya nyumba  yake aliyoshinda  baada ya  kukabidhiwa  leo

 Mshindi  wa  nyumba ya Airtel Yatosha  akionyesha  hati yake ya  nyumba aliyokabidhiwa  leo,huku akiwa na  wafanyakazi  wenzake  waliofika  kushuhudia 

Ofisa mahusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando akimkabidhi mke  wa mshindi  wa  nyumba ya Airtel yatosha Bw  Sylivanus Juma Wanga Bi Veronica Wanga huku kushoto mume wake ambae ni mshindi akishuhudia mshindi  huyo ni mhasibu  wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TARWOC inayojihusisha na mapambano dhidi ya ukatili  wa kijinsia mkoa wa Iringa ,wengine pichani ni wafanyakazi  wenzake waliofika kushuhudia  hafla  hiyo  iliyofanyika Hotel ya M.R mjini Iringa 
 ......................................................................................

•    Kusafirishwa na Airtel kuja dar alhamisi 
wiki hii kupokea nyumba yake
                
Hatimaye mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha yenye thamani 
ya shilingi milioni 65/- iliyotolewa na Kampuni ya mitandao ya simu za 
mkononi Airtel, mwishoni mwa wiki hii amekabidhiwa rasmi funguo yake 
baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni maalumu ya Airtel yatosha 
shinda nyumba 3.

Huku  wananchi  wa  mji  wa Iringa wakijipanga  barabarani  kumshangilia na kuipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa  kuonyesha njia kwa makampuni mengine. Makabidhiano ya funguo hiyo kwa mshindi, Bw. Silvanus Juma yalifanyika 
mwishoni mwa wiki hii mkoani Iringa na kushuhudia mshindi huyo wa 
Airtel akikabidhiwa funguo pamoja na cheti kinachoonesha kwamba yeye 
ni mshindi wa kwanza wa nyumba katika nyumba tatu zinazoshindaniwa 
kupitia promosheni ya Airtel Yatosha.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema hafla  hiyo ya kukabidhi funguo imefanyika  ikiwa  sambamba ya  kumtembelea mshindi  huyo  nyumbani kwake eneo la Frelimo mjini Iringa ili kujionea maisha  yake kabla ya  kukabidhiwa  nyumba yake.

“ makabidhiano ya hizi funguo ni ya awali lakini Alhamisi ya wiki hii
mshindi huyu Bw. Silvanus Juma atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo 
maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam”

Aliendelea kwa kusema Airtel inayo furaha kubwa kumkabidhi mshindi wao 
huyo zawadi hiyo na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja
wake nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na
Kampuni hiyo.

“Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na
hii sio kikomo bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi
nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali
vinavyopatikana kwenye promosheni hii ya ya Airtel yatosha shinda
nyumba 3. mbalimbali za Airtel ili kushinda,” alisema Mmbando.

Aliongeza Mmbando kwamba ili mteja wa Airtel aweze kujiunga na
vifurushi hivyo anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha
aweze kujiunga na kifurushi chochote cha wiki, siku au mwenzi hiyo ndo
njia pekee ya kushinda.

Mpaka sasa  Airtel imeweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake
nchi nzima ambapo imetoa shilingi milioni 37  kwa washindi 37 na
inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90, sambamba na 
hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni bado zinashindaniwa
kupitia promosheni hiyo ya Airtel yatosha, shindanyumba 3.

Akielezea furaha yake Bw. Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati
ya kipekee ambayo hakuitarajia hapo awali na hata alipopigiwa simu
hakuamini kwa sababu alijua kitu kama hicho hakiwezekani na hawezi
kupata nyumba katika msimu kama huo.

“Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu
kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini.

Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na ni kielelezo wazi kuwa
Airtel ni mtandao unaojali na kuthamini wateja wake,” alisema Juma.

Bw Juma alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika
makao makuu ya Airtel Dar es salaam mwisho wa mwenzi wa saba mwaka huu 
ilyopelekea Bw. Juma kuibuka mshindi wa kwanza katika promosheni hiyo.

Wakati  huo  huo baadhi  ya  wananchi  wa mji  wa Iringa katika maeneo  mbali mbali ambayo msafara  wa mshindi  huyo  ulipita  walionekana  kujipanga  barabarani  kumshangilia mshindi  huyo na Airtel  kwa  kumpungia mikono, huku  baadhi ya  shughuli  zikisimama kwa shauku ya kumuona mshindi  wa nyumba ya kwanza  ya Airtel Yatosha  kutoka mjini Iringa.

Akizungumza kwa  nibaya  ya  wananchi wenzake Pendo  Luwoga  alisema  kuwa wamelazimika  kufika  kushuhudia tukio  hilo kutokana na  wengi  wao  kutokuwa na imani na bahati nasibu mbali mbali zinazochezeshwa na makampuni ya  simu ila kwa tukio  hilo la Airtel kweli  wameamini  kuwa hakuna ubabaishaji na  wao  wapo tayari  kujiunga na Airtel na kuendelea  kucheza mchezo  huo ili  ikiwezekano mkoa  wa Iringa  kuonyesha maajabu kwa kushinda nyumba zote.

No comments:

Post a Comment