Thursday, August 15, 2013

BENKI YA CRDB YAZINDUA MIKOPO YA NYUMBA 'JIJENGE'


 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina ya ‘Jijenge’ itakakayoanza kutolewa na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa benki ya CRDB anayeshughulikia mikopo ya nyumba 'Jijenge,' Silas Katemi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo.
 Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa na waalikwa katika hafla hiyo.
 Maofisa wa CRDB.
 Baadhi ya wageni waalikwa. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Saugata Bandyadhiyay.
 Maofisa wa CRDB katika uzinduzi huo.
Dk. Kimei akipiga makofi baada ya kuzinduliwa kwa mikopo ya nyumba 'JIJENGE'
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akibonyeza kitufe cha kompyuta  wakati wa uzinduzi wa mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina ya ‘Jijenge’ itakakayoanza kutolewa na benki hiyo hivi karibuni. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Saugata Bandyadhiyay na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma Kwa Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa. wakibonyeza kitufe cha kompyuta
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongoza waalikwa katika chakula.
 Meneja Uhusiano wa CRDB, Godwin Semunyu (wa pili kulia) na Meneja Uhusiano wa Akaunti ya Tanzanite, Lucy Naivasha (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
 Tumaini Kamuhanda (kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wenzake wa CRDB.
BENKI ya CRDB, leo imezindua mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina la ‘Jijenge,’ itakayoanza kutolewa hivi karibuni na benki hiyo, ili kuwawezesha wafanyakazi, wajasiriamali na hata wakulima kukopa kwa ajili ya ujenzi wa makazi bora ya kisasa.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei, alisema CRDB inajisikia fahari kuleta ufumbuzi suala muhimu katika maisha ya mwanadamu, ambalo ni makazi bora nay a kisasa.

Aliongeza kuwa, kumiliki nyumba ni hitaji muhimu sana la binadamu, linalochangia kumpa heshima na utulivu wa akili na fikra, hivyo kumpa msukumo wa kufanya kazi kwa bidii na kuchangia ufanisi na tija kwa mtu mmoja na taifa kwa ujumla.

Alibainisha kuwa, tafiti zinaonesha kwamba Tanzania ina upungufu wa nyumba zaidi ya milioni 3 ili kukidhi mahitaji, lakini baya zaidi ni ukweli kuwa hitaji la nyumba linaongezeka kwa kiwango cha nyumba 200,00 kwa mwaka, hivyo kunahitajika nguvu za ziada kukabiliana na changamoto hiyo.

Dk. Kimei aliongeza kuwa, juhudu mbalimbali zimefanywa ili kutafuta suluhisho la makazi bora nay a kisasa, lakini kuna changamoto kadhaa zinazokwamisha harakati hizo, zikiwamo za kupanda kwa gharama za kumiliki ardhi na vifaa vya ujenzi kama nondo, mabati na saruji.

Changamoto hizo, pamoja na ile ya kukosekana kwa mfumo thabiti wa kifedha wa kusaidia sekta ya ujenzi, kumesababisha wanachi kufanya ujenzi wa kuungaunga, ujenzi ambao huzaa nyumba zisizo za kisasa wala ubora na kuongeza idadi ya nyumba zisizomalizwa ‘mahame.’

Aliongeza kuwa, mfumo wa ujenzi wa kutumia akiba wanazojiwekea wananchi ni wa kizamani, ambao tayari dunia ya kisasa, hasa katika nchi zilizoendelea zimeshaachana na mfumo huo kutokana na ukubwa wa athari zake kwa jamii na mataifa yao.

Moja ya athari hizo ni kuzifanya familia kuishi maisha ya kujibana sana, hivyo kupunguza ‘Quality of Life,’ kuchochea vitendo vya rushwa miongoni mwa wafanyakazi wanaojaribu kwa kila mbinu kutafuta pato la ziada kumudu kuendesha familia na ujezni kwa pamoja.

Dk Kimeo kafichua kuwa, kwa kutambua hayo, ndio maana CRDB ikaratibu na kisha kuzindua mfumo wa mikopo ya nyumba ya ‘Jijenge,’ unaowaruhusu wateja wa benki hiyo kukopa pesa na kufanya ujenzi bora na wa kisasa, kisha kurejesha taratibu.

Alisisitiza kuwa, mikopo ya ‘Jijenge,’ inawalenga Watanzania wote kutoka sekta mbalimbali, kuanzia wafanyakazi, wajasiriamali, wafanyabiashara na hata wakulima, ambapo kupitia mikopo hiyo, mteja atakopa ili kukarabati, kununu ama kujenga nyumba mpya.

2 comments:

  1. HONGERENI SANA CRDB BANK, HILI NDIO WATEJA WENU TUIALIKUA TUKILISUBIRIA KWA MUDA MREFU SANA.

    HONGERA SANA KWA KUANZISHA TUJENGE LOAN, MTAOKOA MAISHA YA WATEJA WENU WENGI SANA.

    ReplyDelete
  2. Hii habari si ingeambatanisha taarifa au dondoo kidogo jinsi itakavyofanya kazi, riba, qualification etc?

    ReplyDelete