Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa pili kulia akitoa akiitambulisha familia ya marehemu diwani Idd Chonanga aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli aliyefariki dunia jana
Mtoto mkubwa wa marehemu Idd Chonanga Bw Greyson Chonanga akipewa mkono wa pole na waziri mkuu Mizengo Pinda aliyefika nyumbani kwao eneo la kijiji cha Nduli kuhani msiba huo jioni ya leo. Anayeshuhudia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
Viongozi mbali mbali wa CCM na serikali mkoa wa Iringa wakiwa na waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na waombolezaji wa msiba wa aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana
Mtoto mkubwa wa diwani Chonanga akitoa maelezo kwa waziri mkuu Pinda juu ya kifo cha baba yake
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiomboleza msiba wa diwani Chonanga leo katika kijiji cha Nduli Iringa mjini
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiwaaga waombolezaji leo
Waziri mkuu akiaganga na familia ya marehemu Chonaga leo kijiji cha Nduli Iringa mjini
Mtoto mkubwa wa marehemu Chonanga akimuongoza waziri mkuu na msafara wake kuondoka eneo hilo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akiwapa pore wafiwa
Waziri Pinda akiwapa pore wafiwa leo katika msiba wa diwani wa kata ya Nduli mjini Iringa Idd Chonanga aliyefariki dunia jana
Ndugu wa diwani Chonanga wakiangana na waziri mkuu Pinda
Waziri Pinda akiagana na famili ya marehemu Chonanga leo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma kushoto akiwa na mke wa waziri mkuu mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa CCM mjini Iringa
Mwenyekiti wa CCM mjini Iringa Abed Kiponza akimng'ata sikio mama Tunu Pinda
Familia ya marehemu Chonanga akifurahia baada ya kutembelewa na waziri mkuu
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiwapa pore wafiwa leo kamanda huyo aliongozana na waziri mkuu Mizengo Pinda mlezi wa CCM mkoa wa Iringa leo
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas akiwa na familia ya Chonanga na wakazi wengine wa Nduli leo
Msafara wa waziri mkuu Mizengo Pinda ukitoka kuhani msiba wa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana na kuzikwa kesho kijijini hapo.
Wahudumu wa Ndege iliyomleta waziri mkuu wakijiandaa kuagana nae |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akimpokea waziri mkuu Mizengo Pinda |
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba akimpokea waziri mkuu |
|
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Gerald Guninita akisalimiana na waziri mkuu |
Ofisa wa magereza Iringa akimpokea waziri mkuu |
kada wa CCM mzee My Studio akisalimia na waziri mkuu |
Jembe la manispaa ya Iringa mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa Teresia Mahongo akimpokea waziri mkuu Mizengo Pinda kwa tabasamu kali |
Meneja wa Tanroads mkoa wa Iringa ambae anafanya makubwa katika barabara ya Iringa - Dodoma Paul Lwakurwa akipongezwa na waziri mkuu kwa kazi nzuri |
Makada wa CCM kutoka vyuo wakimpokea waziri mkuu pichani na Bwana Alcard |
Makada wa CCM familia ya My Studio |
Wadau wa masuala ya utalii mkoa wa Iringa ambao wanapigania kuitangaza hifadhi ya Ruaha na hifadhi za kusini |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo JOseph Muhumba akisalimiana na waziri Pinda |
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiteta jambo na waziri mkuu Mizengo Pinda katika uwanja wa Ndege Nduli leo |
Picha na habari na Francis Godwin
WAZIRI mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa jioni ya leo amewasili mkoani Iringa na kufika nyumbani kwa aliyekuwa diwani wa kata ya marehemu Idd Chonanga na kuungana na waombolezaji katika kuifariji familia ya diwani huyo.
Waziri Pinda ambae aliongoza na mkewe mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa CCM mkoa wa Iringa pamoja na viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma walifika nyumbani kwa marehe mu Chonanga eneo la Nduli majira ya saa 10.56 na kutumia muda wa zaidi ya dakika 10 kuifariji familia hiyo.
Akiwa nyumbani kwa marehemu Chonanga waziri Pinda na mkewe wametoa pore kwa familia hiyo ya Chonanga na kuwaomba kuendelea kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na kuwa wao katika chama wapo pamoja na familia hiyo katika maombolezo hayo .
Waziri Pinda amesema kuwa binafsi kama mlezi wa CCM mkoa wa Iringa ameguswa na kifo cha diwani Chonanga na kuwa kutokana na kuwa katika ziara ya kichama mkoa wa Iringa ameona ni vema kabla ya kuanza shughuli za chama kufika kuhani msiba huo .
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema kuwa CCM wilaya ya Iringa mjini na mkoa kwa ujumla wamepata pigo kubwa kwa kifo cha diwani huyo na kusema kuwa CCM itashiriki kwa asilimia 100 mazishi hayo yatakayofanyika mapema kesho katika kijiji hicho cha Nduli.
Kwa upande wake Greyson Chonanga ambae ni mtoto wa marehemu Chonanga ameeleza kufurahishwa na hatua ya waziri mkuu kufika kuhani msiba huo na kuwa wao kama familia hawakutambua kuwa msafara mkubwa kama huo wa kitaifa ungefika kuhani msiba huo.
Huku wakazi wa eneo hilo la Nduli wameelezwa kufurahishwa na umoja wa kweli uliopo ndani ya serikali ya CCM kutokana na viongozi wake kuwajali watu wa chini wanaowaongoza na kuwa utu ambao waziri mkuu ameonyesha ni upendo tosha kwa wana Nduli kwa serikali ya CCM.
Alisema Adam Kalinga mkazi wa kata hiyo ya Nduli ambae alikuwepo msibani hapo kuwa katika kuenzi kazi za marehemu Chonanga wao wataendelea kutambua mchango wake .
Kupeana pole ni wajibu kwani hilo si ls mmoja tuko hapa duniani kwa muda tu sote ndo njia yetu hiyo. Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi.Ameen
ReplyDelete