Sunday, July 14, 2013

TAHA yafungua rasmi ofisi zake za Zanzibar

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo na Maliasili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak akihutubia wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa ofisi hizo za Tanzania Horticultural Association (TAHA) 
Mkurugenzi wa TAHA, Bi Jacqueline Mkindi akisema neno la ufunguzi kwa Mh. Mtumwa Kheir Mbarak na wageni waharikwa wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa Ofisi za TAHA-Zanzibar
Moja ya mashamba darasa ya TAHA yaliyopo eneo la Donge, Wilaya ya Kaskazini Unguja.
Wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha Mazao ya horticulture wakiwa katika moja ya Warsha zilizoandaliwa na TAHA masaa machache kabla ya ufunguzi wa ofisi hizo kisiwani hapo.
Baadhi tu ya pilipili bora zinazolimwa na wakulima wanachama wa TAHA, mazao haya yenye afya ni matokeo ya elimu za kilimo bora zinazotolewa na wataalamu wa TAHA visiwani humo.
Hili ni soko la Darajani Zanzibar, ni baadhi tu ya maeneo ambayo bidhaa za wakulima wa horticulture Zanzibar upelekwa na kuuzwa kwa ajili ya kukizi haja za soko la ndani.
Mkurugenzi wa TAHA akiteta Jambo na Mtaalamu wake kwa upande wa Visiwani Mzee Biwi wakati alipotembelea moja ya mashamba ya tikiti maji ya wakulima ambao ni wanachama wa TAHA.
Wataalamu kutoka Finland ambao ndio wawezeshaji wa shughuli za TAHA Zanzibar wakitazama moja ya shamba la Matikiti maji la moja ya vikundi wanachama wa TAHA.




Ukiwa na swali hoja na maoni ingia hapa uwasiliane nao leo TAHA

Taasisi kilele ya TAHA inayoundwa na wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha 'horticulture' nchini Tanzania hatimaye imefungua rasmi ofisi zake kuu katika visiwa vyenye marashi ya karafuu Zanzibar. Ufunguzi wa ofisi hizo zilizo mtaa wa Kikwajuni kwenye Jengo la mfuko wa barabara ulitanguliwa na ziara fupi ya kutembelea maeneo ambayo Taasisi hiyo imeanzisha mashamba darasa na kusajili vikundi vya wakulima ili waweze kufaidika kwa karibu zaidi na ushauri wa kiufundi katika masuala ya kilimo cha 'horticulture' hali kadhalika masoko ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment