Mr. Yusuph Kileo (Cyber
Security and Digital
forensics Investigations Expert)
|
Na Yusuph Kileo.
Hivi karibuni kwa takriban miezi miwili kumekua na midahalo mbali mbali ambayo imekua ikiendelea katika nchi nyiingi na nimepata kuhudhuria kama mwanachama wa kudumu wa kikundi kinacho jihusisha na maswala ya Ulinzi mtandao katika nchi za Africa.
Aidha
ripoti iliyowasiilishwa na ITU huko Geneva
ilisema, kumekua na ongezeko kubwa la madhara ya mtandao ambapo
ilielezwa mitandao imekua ikiathiriwa zaidi kwa Asilimia 30, “Phishing Sites
spoofing social networks” imeongezeka kwa asilimia 125 na kuelezwa nusu ya
vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17 uliimwenguni kote wamekua
wakiathirrika na kilichotambulishwa kama “Cyberbulling”.
Vile
vile Tafiti zilizo wasilishwa katika ripoti ya “the World Federation of Exchanges and the
International Organization of Securities Commissions” zime eleza nusu ya taasis za fedha duniani zimeweza kuathirika na “Cyber-attacks” pamoja na wizi mtandao hadi kufikia mwaka jana mwishoni huku ikielezwa kushindikana kutatua hali hiyo kwa takriban robo nzima ya taasisi hizo za fedha dhidi ya tatizo hilo.
International Organization of Securities Commissions” zime eleza nusu ya taasis za fedha duniani zimeweza kuathirika na “Cyber-attacks” pamoja na wizi mtandao hadi kufikia mwaka jana mwishoni huku ikielezwa kushindikana kutatua hali hiyo kwa takriban robo nzima ya taasisi hizo za fedha dhidi ya tatizo hilo.
Hayo
na mengine mengi ambayo yamepata kujadiliwa kwa kina yalionekana kuwa ni
changamoto kubwa katika dunia ya sasa ambapo kutakua na ugumu sana kukimbia
utumiaji wa teknologia katika maisha yetu yakila siku. Kwa sasa hali ya
utumiaji wa mitandao kuongezeka nchini katika sekta mbali mbali kuanzia kufanya
miamala ya biashara hadi katika sekta za elimu na maeneo mengine mengi.
Wimbi
kubwa nchini limeongezeka la watu kuwa na matumizi mabaya ya mitandao ambapo
imekua ikileta athari kubwa kwa jamii katika maeneo mengi hasa yaki biashara
lakini pia hata kutishia hali ya usalama wanchi kwa kusambazwa maneno mbali
mbali ya kutishia Amani ya nchi kwa kipindi kifupi tofauti na awali wakati
matumizi ya mtandao hayakua na ongezeko lililoko sasa.
No comments:
Post a Comment