Tuesday, July 9, 2013

Kongamano la kiislam la kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhan lafanyika jijini dar

Mbunge CCM Al-Shaymaa Kwegyir akichangia ambapo aliitaka Jamii kumlea vizuri na kimaadili Mtoto wa Kike kwani mtoto wa kike akilelewa vyema ndio nguzo ya familia Kimaadili na wakati sahihi wa kumjenga kama nguzo ni kuanzia utotoni.
Katibu Mkuu wa Jumuia na Taasisi za Kiislam Sheikh Ramadhan Sanze akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari juu ya Changamoto na Maendeleo Mbali Mbali Jamii ya Kiislamu ya Tanzania hasa wanawake inayopiga wakati wa Kongamano.
Wanataaluma Wa Kiislam wakifuatilia kwa Makini Mada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan iliyowasilishwa na Sheikh Suleiman Amran Kilemile wakati wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan.
Wanataaluma Mbali mbali wa Kiislamu wakimsikiliza kwa makini Ustaadh Bakari Kombo Bakari kutoka Zanzibar alipokuwa akiongelea nafasi ya Muislam Mwanamke Wakati wa mtume Muhammad (SAW), Kabla yake na Mazingira ya Mwanamke leo.
Washindi wa zawadi za Utendaji uliotukuka 1434 kutoka kwa Wanataaluma wa Kiislam Tanzania wakati wa Picha ya Pamoja na Wenyeviti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Shk Kilemile pamoja na Rais wa Wanataaluma Waislam Bro. Mussa Mziya. Kutoka Kushoto ni Mussa Mziya (TAMPRO), Sheikh Arif (Islamic Foundation), Sheikh Mohamed Said (Independent Author), Sheikh Ramadhan Sanze (Baraza Kuu), Sheikh Suleiman Kilemile (Hay’at), Sheikh Jabir Katura (Msikiti Mkuu Mwanza) na Hajat Aisha Sururu (Aisha Sururu Foundation).
Bi. Riziki shahari akimkabidhi Bi Aisha Sururu zawadi pamoja na pesa kuwakilisha wanawake wanaojituma kusukuma mbele mambo ya Kijamii na kutunza Maadili Bora kwenye Umma.
Sheikh Jabil Katura kutoka Mwanza alipokabidhiwa Zawadi yake Pamoja na Pesa Akiwakilisha Kundi la Masheikh wenaosimamia vyema Waislam. Pamoja nae ni Shk Kilemile, Mwenyekiti wa wanazuoni wa Kiislam Tanzania, na Bw. Mussa Mziya Rais wa Wanataaluma Waislam Tanzania.
Zaidi ya wanataaluma 400 walikutana na kujadili Mchango wa Mwanamke wa Kiislam katika kujenga mafanikio ya jamii Kiroho, Kiuchumi na Kijamii kwa Ujumla ambapo Kauli Mbiu ya Mwaka 2013 ilikuwa “Mwanamke ni Nguzo Katika Maendeleo ya Jamii”.
Mbunge Al-Shaymaa Kwegyir akipata Maelezo Kutoka kwa Afisa wa Huduma za Benki ya Kiislam ya Amana wakati akifungua akaunti, Amana Bank ndio Wadhamini wa Kongamano la Wanataaluma wa Kiislam la Kukaribisha Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani Mwaka 2013 lililofanyika Hotel ya JB Belmonte – Dar es Salaam.



1 comment:

  1. Masha Allah, this was one Great Islamic Corporate event. Wish to have more of these event in town.

    ReplyDelete