Sunday, July 7, 2013

KATIKA KUADHIMISHA SIKUKUU YA SABASABA, WANABIAFRA WAKIMBIA ZAIDI YA KILOMITA 8

Kama ilivyo ada ya kila jumapili kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) pamoja, leo Wanabiafra wamekimbia zaidi ya kilomita nane katika kuadhimisha sikukuu ya saba saba. Mbio hizo zilianza majira ya saa 12:25 asubuhi yalipo makao makuu ya klabu kupitia barabara ya Kawawa hadi Moroko, barabara ya Kibaki hadi kwa Mwalimu Nyerere, barabara ya Rose Garden Hadi Sayansi, brabara ya Maji Machafu na kufuata barabara ya Akachube mpaka Peace Mwananyamala, barabara ya kwa Kopa, barabara ya Dunga hadi Hombus kisha barabara ya Kawawa hadi Msikiti wa Mtambani tukaingia "service road" ya upande Kinondoni Hospital mpaka Manyanya (Chimbinga) ambapo mbio ziliishia. Fuatilia matukio kwa picha mbalimbali!
Maeneo ya kwa Nyerere


Barabara ya kuelekea Rose Garden




Add caption









Mwana- mzimuni Jogging (mwenye fulana ya kijani) aliungana na Wanabiafra kwenye mazoezi



Tukivuka mataa ya Sayansi kuelekea maji machafu

  
Tunawashukuru sana askari wa usalama barabarani (traffic) kwa kutambua mazoezi yetu, mara zote wamekuwa wakituwezesha kutumia na kuvuka barabara hasa sehemu zenye mataa kwa kusimamisha magari mpaka tunapopita. Leo wakati tukivuka njia panda ya sayansi, askari wa usalama barabarani alisimamisha gari zote tukiwa umbali wa takriban mita moja na nusu kabla ya kufika kwenye mataa. Tulivuka salama na kuendelea na mazoezi.

Watoto wakifurahia mazoezi kwa tabasamu

Tukinyoosha miguu na kupanga vyema mistari maeneo ya Akachube


Tukikatiza kuingia barabara/maeneo ya Peace - Mwananyamala



Tukinyoosha viungo baada ya kufika Chimbinga



Mwanachama mpya Bw. Khamis Seif (mwenye jezi nyekundu - aliyesimama) akitambulishwa





Watoto wakipata staftahi ya chai baada ya mazoezi
  
Rehema Shabani (kushoto) na Miriam Jospeh (kulia) baada ya mazoezi wakipata habari

Wanachama wapya Boniface (kushoto) na Hassan (kulia)



Wanabiafra wakiangalia picha za matukio ya jogging leo
Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, tunawapongeza Wanabiafra wote walioshiriki mazoezi siku ya leo na kusisitiza pia kuwahimiza wanachama wengine, ndugu, jamaa na marafiki zetu washiriki mazoezi ili kujenga afya zao.

No comments:

Post a Comment