Thursday, July 18, 2013

BARAZA KUU LA USALAMA LA JADILI USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI


Na  Mwandishi Maalum

Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa, jana jumatano liliendesha majadiliano ya wazi kuhusu usalama wa waandishi wa habari katika  maeneo  yenye migogoro.
Majadiliano hayo yaliratibiwa na Marekani ambaye ni  Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Julai, na kuhudhuriwa na waandishi wanne  wa kimataifa  ambao  walipata fursa ya  kuelezea masahibu wanayokumbana nayo  wakati wa kitekeleza majukumu yao.
Majadiliano kuhusu  suala la usalama wa waandishi wa habari katika maeneo yenye migogoro ni ya kwanza kufanyika ndani ya  Baraza hilo, tangu  lilipopitisha Azimio namba 17 38 mwaka 2006 lililokuwa likizungumzia  suala hilo. Aidha hii pia ni mara ya kwanza kwa waandishi wa kimataifa kuzungumza ndani ya Baraza Kuu la Usalama.
“ Hapa nilipo  mimi ni maiti anayetembea  ,   ninatembea   pasi kujua nani anaweza kuondoa  uhai wangu,wakati wowote naweza kupotea maisha.  naweza kuuawa  hata na kijana mdogo    ilimradi ana silaha”
Kauli hiyo ilikuwa ni ya Bw. Mustafa Haji Abdinur anayeandikisha  AFP akitoka Somalia.  Na kuongeza kwamba rafiki zake wengi ambao ni waandishi wenziye tayari  wameshapotea maisha  na kwamba kwa yeyé kuwa hai mpaka sasa ni  kama bahati lakini ni suala la wakati tu.
Naye  Bi. Cathleen Carrol  ambaye ni  Mhariri Mtendaji wa Associated Press na Makamu  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya    Kuwalinda Waandishi ( CPJ) pamoja na kuelezea  kwa uchungu mkubwa  matukio ya mauaji yaliyowakumbua waandishi wenzake katika  maeneo mbalimbali duniani  anasema, katika  shirika lao  kuna eneo ambalo  limetengwa maalum kwaajili ya kuwaenzi waandishi wote ambao wamepoteza maisha katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake,  mwandishi Richard Engel wa NBC news, yeyé pamoja na kuelezea  mikasa mbalimbali ambayo amekwisha  kumbana nayo yakiwamo ya kutekwa wakati akiripoti matukio ya migogoro, yeyé alikwenda mbalia zaidi kwa kuuliza ni nani hasa mwandishi wa habari.
Bw, Engel alieza kwamba ulinzi wa waandishi wa habari hivi sasa unakuwa mgumu  sana tofauti na miaka  ya nyuma kutokana na kile alichosema kuibuka kwa makundi mengi yanayofanya kazi za  waadishi wa habari.
“ Wakati tukijadili  hoja hii ya  usalama wa waandishi wa habari, pengine pia ni muhimu tukajiuliza hivi ni nani hasa mwandishi wa  habari,  je mwanaharakati anaye shika  video au kamera na  kalamu je naye ni mwandishi,  au je na yule  mwanamgambo mwenye silaha lakini naye ameshika  kamera na kupiga picha  je naye   ni mwandishi” akahoji Bw, Engel
Anasema kwamba ni jambo la kawaida hivi  unapokwenda kwenye tukio fulani  kukutana na makundi ya watu kila mmoja akiwa ameshika kamera yake akichukua matukio, na katika mazingira kama haya,  ni vigumu kwa vyombo vya ulinzi na  usalama kutofautisha nani hasa ni mwadishi aliyesomea na kubobea kwenye fani hiyo na yupi  mwanarakati.
Kwa maoni yake anasema  pamoja  na hamu ya kila mtu kutaka kutaka kukukusanya habari na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii,  ni vime kujiuliza  nani anastahili na anapwashwa kupewa ulinzi anapotimiza majukumu yake na kwa vyovyote vile anasema kama ilivyo kwa wanadiplomasia ambao wanakinga vilevile waandishi waliosomea na wenye weledi na taaluma yao wanatakiwa kupewa ulinzi.
Majadiliano hayo yalifunguliwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson,  na yalikuwa na mvuto wa ina yake  hasa kutoka na kauli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wachangiaji.
Kwa upande wake  Naibu Katibu  Mkuu alieleza kwamba  hujuma dhidi ya waandishi wa habari ni jambo lisilokubalika kwa kile alichosema ni kubinya  uhuru wa  upatikanaji na utoaji wa habari, lakini pia ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza. Akalipongeza  Baraza kwa kuitisha mjadala huo
Akasema  karne iliyopita waandishi wa habari wapatao 600 walipoteza maisha katika matukio mbalimbali  na wengine wakiishia magerezani, huku asilimia 90 ya matukio hayo hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa.
Pamoja na wachangiaji wengi kukiri kwamba  mazingira ya  ufanyaji kazi kwa waandishi wa  habari yamezidi kuwa magumu na hatari,  walielezea pia  kwamba mazingira hatarishi  hayapo tu katika maeneo yenye vita bali  hata katika nchi wazofanyia kazi. Ambapo takwimu kutoka  CPJ zinaonyesha  katika kila waandishi  watano kati ya sita wanauliwa wakiwa ndani ya nchi zao.
Wengi wa wazungumzaji walieleza kwamba  baadhi ya waandishi ama wamekuwa wakitishiwa maisha yao  na familia zao au hata kupoteza maisha  kwa kuandika  na kuchapicha habari zinazofichua  vitendo vya rushwa , vitendo vya jinai au kashfa zinazohusu makundi mbalimbali ya jamii na  vilevile kuandika habari za uchochezi  kati ya  kundi moja na jingine..
Wengine wakaenda mbali kwa kusema  wakati mwingine waandishi wenyewe wanajiweka katika mazingira ya hatari kwa kukiuka misingi ya kazi zao, kwa kuandika habari zinazopendelea  upande mmoja, au kufanya kazi kinyume cha  matakwa na matarajio ya yule anayemfanyia kazi.
Wazungumzaji hao wakatoa wito kwa  Baraza kuu la Usalama kuangalia namna  bora ya kuboresha ulinzi wa waandishi wa habari katika mazingira  hatarishi kama vile vita na migogoro na pia wakatoa wito wito  kwa waandishi wa habari kuzingatia  misingi ya taaluma zao na kuepuka kujingiza katika mitengo isiyo  ya lazima.
Suala lingine lililozungumwa kwa  kina ni lile la kutofikishwa mbele ya mkono wa sheria watu wanaotuhumiwa  kuwahujumu waandishi wa habari.


No comments:

Post a Comment