Sunday, June 16, 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA KITABU CHA SUMBAWANGA NG'ARA KILICHOANDIKWA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha "Sumbawanga Ng'ara" kilichoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (wa katikati) katika ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma, kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa. Kitabu hicho kinaelezea na kutoa muongozo juu ya usafi na uhifadhi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kitabu hicho kinauzwa Tsh. 3,500 kwa lengo la kukusanya fedha ya kuchapisha machapisho mengine zaidi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho alitoa wito kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mpango waliouanzisha wa Sumbawanga Ng'ara kwa kuweka mikakati na kutengeneza sheria ndogondogo za kusimamia mpango huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akisoma hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua kitabu cha Sumbawnga Ng'ara ambapo alimshuru kiongozi huyo Mkuu katika nchi kwa kutenga muda wake pamoja na waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi. Zaidi ya vitabu 175 vilinunuliwa baada ya uzinduzi huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitambulisha viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakiwemo baadhi ya mawaziri, wabunge, madiwani kutoka Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wengine wa chama na Serikali.
 Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mzengo Kayanza Peter Pinda akizungumza katika hafla hiyo ambapo alimpongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya kwa kuanzisha mpango wa Sumbawanga Ng'ara pamoja na kuandikia kitabu. Alisema viongozi kama hawa wanaofanya mambo kwa vitendo ndio viongozi wa mfano wanaotakiwa katika taifa letu.

 Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anaeshugulia Elimu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla hiyo. Kwa upande wake alisema kama Wizara wanaipongeza Serikali na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kuanzisha mpango huo wa Sumbawanga Ng'ara na kuunga mkono. Alisema halmashauri zingine zinatakiwa zijifunze kwa kuanzisha mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya utunzaji wa mazingira. Mhe. Majaliwa aliahaidi kununua vitabu 10 vya Sumbawanga Ng'ara.

Mhe. Pindi Chana, Mbunge Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Njombe akizungumza katika hafla hiyo. Alimsifu mwandishi wa kitabu hicho cha Sumbawanga Ng'ara ambaye pia ni muasisi wa mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na kusema ni mchapakazi wa kuigwa. Mhe. Chana aliahidi kununua vitabu 30 vya Sumabwanga Ng'ara kwa ajili ya kuhamasisha usafi Mkoani Njombe.

Mbunge wa Kilindi CCM Mhe. Beatrace Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo ambaye naye alipewa fursa na Waziri Mkuu aweze kuzungumza ambapo alisema Mkoa wa Rukwa umepata kiongozi thabiti ambaye angetamani afanye kazi katika Mkoa wake wa Tanga. Mhe. Selukindo alinunua vitabu 20 kwa ajili ya madiwani wa Korogwe ili awape wivu wa kufanya kazi katika maeneo yao.

 Mama Anne wa UNDP akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu cha Sumbawanga Ng'ara ambapo alifurahishwa na kitendo hicho na kusema yeye pia ni mdau wa mazingira na hivyo akaahidi kununua vitabu 10 kwa ajili ya kuviweka katika maktaba yake.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa akielezea kwa kifupi Mpango wa Sumbwanga Ng'ara ambapo alisema tangu mpango huo uanzishwe na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya wananchi wengi wameupokea vizuri na tayari Mji wa Sumbawanga umeshanza kubadilika ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

 Wajukuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wanaosoma nchini Marekeani wakijitambulisha katika hafla hiyo baada ya kupewa fursa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiendelea na hotuba yake.

 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akimkadhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima kitabu cha Sumbawanga Ng'ara mara baada ya kukizindua rasmi.

No comments:

Post a Comment