Saturday, June 1, 2013

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA KONGAMANO LAKUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU TOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Sierra Leone Mama Sia Koroma muda mfupi kabla ya kuhudhuria kongamano kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV/AIDS kutoka kwa mama kwenda kwa motto. Kongamano hilo lilifanyika kwa ushirikiano wa Japan na Umoja wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Afrika (OAFLA) kwenye ukumbi wa Pacifico Yokohama nchini Japan tarehe 1.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete afifanya mazungumzo na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Ethiopia Madam Roman Tesfaye kabla ya kuhudhuria kongamano kuhusu maambukizo ya HIV/AIDS lililofanyika katika mji wa Yokohama nchini Japan tarehe 1.6.2013.
Wajumbe waliofuatana na Mama Salma Kikwete wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Mke wa Waziri Mkuu wa Japan Madam Akie Abe kwenye wakati wa kongamano.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akihudhuria kongamano kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV/AIDS lililoandaliwa na serikali ya Japan kwa kushirikiana na OAFLA huko Yokohama nchini Japan tarehe 1.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Inkhosikati Nolighwa Ntentesa wakati wa kongamano lililokuwa linajadili kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV/AIDS kutoka kwa mama kwenda kwa motto lililofanyika tarehe 1.6.2013 huko Yokohama nchini Japan.
Picha ya pamoja ya wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika na Japan mara baada ya semina ya siku moja iliyofanyika huko Yokohama nchini Japan tarehe 1.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na Mke wa Rais wa Ghana Madam Lordina Mahama mara baada ya kuhudhuria kongamano kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV/AIDS kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa ushirikiano wa Japan na Umoja wa wake wa Marais na wakuu wan chi za Afrika uliofanyika huko Yokohama nchini Japan terehe 1.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland mara baada ya kuhudhuria kongamano la kuhusu kupunguza maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto lililofanyika nchini Japan tarehe 1.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia jambo na Mke wa Rais wa Cote D’ivoire Madam (kushoto) na Mke wa Rais wa Mali Madam Traore Mentou Doucouri (kulia) mara baada ya kuhudhuria kongamano la kuzuia maambukizi ya HIV/AIDS kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Japan na Umoja wa wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika (OAFLA) huko Yokohama tarehe 1.6.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment