Watanzania wakipunga mikono wakati wa ufunguzi wa mikutano ya watumishi wa umma barani Afrika hapa Nchini Ghana.
Afisa Tawala Mwandamizi wa Wizara ya Fedha Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Merkion Ndofi akimkaribisha mwananchi wa Ghana katika banda la Wizara ya Fedha.
Bw. William Ghump amabaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mkurungezi wa Utawala na Utumishi Bw. Peter Mapigano wa Benki ya Posta Tanzania pamoja Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma wakipanga mkakati wa uelimishaji umma katika banda la Wizara ya fedha.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha Bi. Christina Ngonyani akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa Ghana juu ya umuhimu wa mikopo kwa Watumishi wa Serikalini.
Afisa Tawala Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Merkion Ndofi akiwaeleza wanafunzi wa Ghana juu ya utendaji kazi wa Idara ya Utawala katika wizara ya Fedha Nchini Ghana.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo ya Watumishi wa Umma wa Wizara ya Fedha Bi. Christina Ngonyani akiwa na Afisa Tawala Mwandamizi Bw. Merkion Ndofi , wakitoa ufafanuzi kuhusu utendaji wa kazi za Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali kwa wageni waliotembelea banda la Wizara ya fedha.
Waziri wa Utumishi wa Umma ,Ofisi ya Rais Bi. Celina Kombani na Katibu Mkuu Bw. George Yambesi walipotembelea banda la Wizara ya Fedha hapa nchini Ghana.
Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi Ingiahedi Mduma akifafanua jambo kwa Bw. Eugene Koranteng Henaku wa Umoja wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Serilkali za Mitaa Nchini Ghana.Picha zote na Scola Malinga- Hazina -Tanzania. Picha na GCU-HAZINA -Ghana.
Michuzi hufanyi haki kaka. Tanzania kwenye maonesho hayo imewakilishwa na taasisi 42, lakini wewe tangu juzi unatoa taarifa na picha za Wizara ya Fedha tu. umeshatumiwa picha na maelezo kibao toka taasisi nyingine lakini wewe waiona Wizara ya Fedha tu, au kwa kuwa wao ndio wenye fedha? Kwa taarifa yako, zipo taasisi ambazo zinaibeba Tanzania huku, wewe subiri siku ya kufungwa maonesho utasikia. Tenda haki katika utoaji habari ankal.
ReplyDelete