Sunday, June 30, 2013

JK AWAANDALIA MARAIS DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.

 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akihutubia katika hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku
 Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
 Bendi ya THT ikitumbuiza katika hafla hiyo
 Msanii Mwasiti akipongezwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. Kulia ni Mbunge wa bunge hilo, Shy Rose Bhanji na Abdul Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge hilo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
                                              Kimbisa akiwa na Mwinyi, Bhanji na Richard Kasesera

No comments:

Post a Comment