Friday, May 24, 2013

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAMPONGEZA JAJI ALOYSIUS MUJULIZI BAADA YA KUAPISHWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE KUWA MWENYEKITI WA TUME

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mh. Jaji Aloysius Mujulizi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Waziri wa mambo ya Nje Benard Membe (wa kwanza kulia) akiwa na Mabalozi wateule pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mh. Jaji Aloysius Mujulizi (wa pili kulia) wakati wakisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mujulizi mara baada ya kuapishwa.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Makamishna na watumishi wa Tume.
Watumishi wa Tume wakifurahi wakati wa kumpongeza Mwenyekiti wao Mh. Jaji Aloysius Mujulizi.
Bi. Halima Chawa akimzawadia shada la maua kwa niaba ya watumishi wa Tume Mwenyekiti wa Tume Mh. Jaji Aloysius Mujulizi alipowasili ofisi za Tume mara baada ya kuapishwa.
Kamishna wa Tume Ester Manyesha akizungumza wakati wa kumpongeza Mh. Jaji Mujulizi.
Jaji Mujulizi akiongea na watumishi wa Tume.

Jaji Mujulizi akipongezwa pamoja na familia yake na watumishi wa Tume
Mwenyekiti wa Tume Jaji Mujulizi akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.  (Picha zote na Munir Shemweta LRCT).

No comments:

Post a Comment