Baadhi ya Viongozi, Wajumbe na Wanachama
Wapya katika picha ya pamoja
Mwenyekiti wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Maina Ang’iela Owino
akimkabidhi vitendea kazi ikiwemo katiba ya chama kwa Ndugu Chande
Kigwalilo mwenye kofia Mwenyekiti Shina jipya la Cardiff.
Katibu wa CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Bi. Mariam
Mungula akimkadhi kadi za wanachama wapya Katibu wa shina Jipya la CCM Cardiff
Bi. Rosemary Kiputa.
Mwenyekiti
wa TAWI LA CCM UK Ndugu Maina Ang’iela Owino akiongoza nyimbo za chama katika
shamrashamra za ufunguzi wa shina jipya la CCM CARDIFF WALES.
Wajumbe
wakitega sikio kusikia machache toka kwa Mwenyekiti wa TAWI LA CCM UK
Ndugu Maina Owino hayupo pichani.
Naibu Katibu CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Albert Ntemi, Naibu katibu Itikadi Siasa na
Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa na Bi Rose Kiputa Katibu shina
jipya la Cardiff wakifuatila kwa makini mada muhimu katika ufunguzi huo.
Makamu
Mwenyekiti CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Said Sukwa akitoa yake machache
katika ufunguzi huo.
Wajumbe
wa Shina jipya la CCM Cardiff Wales.
Wajumbe
na wanachama wapya CCM Shina la Cardiff.
Naibu Katibu Itikadi Siasa na Uenezi CCM TAWI LA UNITED KINGDOM Ndugu Abraham Sangiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa Shina la CCM Cardiff Ndugu Chande Kigwalilo na Mjumbe wa Shina la
CCM Cardiff Bi. Prudencia Kimiti.
Viongozi waliochaguliwa Shina la CCM Cardiff wakichukua nafasi zao
aliyesimama na kutoa machache ni Ndugu Chande Kigwalilo Mwenyekiti Shina la CCM
Cardiff akiwashukuru wajumbe kwa kumpa nafasi ya kuongoza shina hilo.
Wajumbe
wa CCM Cardiff wakipeana mkono wa pongezi toka kwa Mwenyekiti CCM UK Ndugu
Maina Owino.
Dr.
Abdallah Saleh Mwenyekiti wa CCM Shina la Northmpton akifafanua jambo katika
ufunguzi huo.
Bi.
Prudencia Kimiti Mjumbe wa CCM Shina la Cardiff akitoa shukrani zake kwa
uongozi wa TAWI LA UNITED KINGDOM kwa kuwezesha ufunguzi wa Shina Jijini
CARDIFF.
Na Abraham Sangiwa
Itikadi Siasa na Uenezi CCM – UNITED KINGDOM
Katika ufunguzi huo uliojaa shamrashamra
na nderemo na kuhudhuriwa na viongozi
wote wa Tawi la CCM UK, Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM Ndg Maina Ang'iela Owino, Makamu Mwenyekiti Ndugu Said Sukwa, Katibu Bi. Mariam Mungula,
Naibu Katibu Ndugu Albert Ntemi, Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu
Leybab Mdegela, Naibu Katibu Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Abraham Sangiwa,
Katibu wa Uchumi na Fedha Ndugu John Juma Lyimo, Naibu Katibu Uchumi na Fedha
Ndugu Mohamed Upete na wanaCCM toka mashina mbalimbali ya CCM UK.
Mwenyekiti wa Tawi la CCM UNITED KINGDOM
Ndg Maina Ang'iela Owino aliwashukuru
Watanzania hao kwa kujitokeza kwa wingi kuandaa, kuyakubali madhumuni na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Ndg Owino
aliwakumbusha kuwa uhalali wa shina lao unajumuishwa katika Sera ya nje
na matawi yake katika Katiba ya CCM.
Ndg Owino aliwakumbusha kuwa kujiunga na
CCM kunaambatana na kuzingatia masharti ya kuheshimu watu, kufanya juhudi za
kuielewa, kuielezea, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM. Pia
kwamba CCM inathamini haki na wajibu wa mwanachama.
Aidha Ndg Owino hakusita kuwakumbusha kuwa
CCM na Serikali yake inaendelea kujijenga na kuboresha taasisi zake ili
kuendana na mahitaji ya kizazi na wakati uliopo na hivyo basi wanaCCM Cardiff wasioneane haya wala kuogopa
kuchagua viongozi wenye sifa za kutosheka na wasio tawaliwa na tamaa na watakao
zingatia miiko ya uongozi kama inavyoainishwa katika katiba ya CCM.
Kabla ya kuhitimisha hotuba yake Ndg Owino
alichambua na kuainisha kwa kina na kuishirikisha halaiki kufanya tathmini ya
wazi ya jinsi CCM imeiongoza serikali kutekeleza ilani yake ya uchaguzi ya
2005/2010 na mafanikio dhahiri yanayopatika katika kutatua kero za wananchi.
Aidha alisema baadhi ya changamoto zilizopo nchini ni matokeo ya mabadiliko
endelevu, kukua na kuendelea kwa mifumo na taasisi za umma na sekta binafsi na
kwamba CCM na serikali yake inaendele kujiimarisha kuyakabili kwa mikakati na
mipango endelevu ya muda mfupi na mrefu, pia Ndugu Maina aliwakumbusha Wana CCM
UK Kuwa mchango wao unathaminiwa na ni wamuhimu katika kuleta mabadiliko
yatayowanufaisha wengi katika nyanja mbalimbali muhimu za kimaendeleo na
kichumi
Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi na ile ya
Uchumi na Fedha walitoa machache yanayohusu idara zao na namna zinavyofanya
kazi ili kuwapa mwanga wanachama wapya na viongozi katika shina hilo.
Ufunguzi huo ulifuatiwa na uchaguzi wa
Viongozi mashina uliosimamiwa na Katibu wa CCM UK, Bi Mariam Mungula.
Viongozi waliochaguliwa katika shina hilo
jipya la Cardiff – Wales ni;
- Chande Kigwalilo Mwenyekiti wa Shina
- Bi. Rosemary Kiputa Katibu wa Shina
- Prudencia Kimiti Mjumbe wa Shina
- Munde Nyirambo Mjumbe wa Shina
- Alen
Mguto Mjumbe wa Shina
Mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa shina jipya la Cardiff Ndugu
Chande Kigwalilo alitoa machache na kushukuru wajumbe na wanachama kumpa nafasi
ya kuliongoza shina na kushukuru uongozi wa tawi kwa kufanikisha ufunguzi huo
na kuwakarakibisha Jijini Cardiff.
Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na
Uenezi
CCM TAWI LA UNITED KINGDOM
Sasa CARDIFF kimeeleweka changamoto bado zipo kwani kuna mambo mengi tunahitaji kuisadia serikali yetu kufanya mabadiliko na kwenda na wakati katika uchumi endelevu
ReplyDelete